Home SPORTS RANI YAMJAZA MAPESA NYOTA WA SIMBA QUEEN

RANI YAMJAZA MAPESA NYOTA WA SIMBA QUEEN

NA: MWANDISHI WETU 

MDHAMINI mwenza wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, Rani Sanitary Pads (Taulo za kike) wamemkabidhi mshambuliaji wa Simba Queen, Opa Clement tuzo ya Mchezaji bora wa Mwezi Januari na kiasi cha pesa Sh. Laki Tano.

Opa ambaye mshambuliaji kinara wa Simba Queen amepewa kiasi hicho cha pesa pamoja na tuzo katika mechi yavtinu yake dhidi ya Fountain Gate ya Dodoma iliyofanyika katika uwanja wa MO Arena na wao wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Opa alisema amefurahishwa na tuzo hiyo na kusema itaongeza hamasa ya ushindani katika ligi.

“Binafsi nimependa hiki kitu maana kitaongeza hamasa ya kupambana ndani ya ligi yetu.

“Hivi sasa kila mchezaji atataka kushinda tuzo hii na hii itachangia kuongeza ushindani mkubwa ndani ya ligi yenyewe” alisema Opa.

Mratibu wa Rani Sanitary Pads Abdulah Mkeyenge alisema wameamua kutoa tuzo hizo ili kuuheshimisha mpira wa kina mama nchini.

“Sidhani kama tuliwahi kuwa na kitu cha namna hii katika mpira wetu wa kina mama huko nyuma, hivyo unavyoona Rani Sanitary Pads tuko hapa ni kutaka kuupa thamani mpira huu ambao bado hauna hamasa kubwa kama mpira wa kiume” alisema Mkeyenge.

Katika hatua nyingine Rani Sanitary Pads imewapa zawadi zao za taulo hizo timu ya Fountain Gate.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here