Home ENTERTAINMENTS MSANII NAGWA KUACHIA NGOMA MPYA

MSANII NAGWA KUACHIA NGOMA MPYA

NA :MWANDISHI WETU

Nyota wa muziki wa Singeli na muigizaji Hamilton William ‘Nagwa’, amefunguka kuachia ngoma mpya ambayo itakuwa kwenye maudhui ya Bongo Fleva.

Msanii huyo kwa sasa ana tamba katika tamthilia ya Mwanamziki inayoruka katika chanel ya Sinema Zetu ambayo inaeleza maisha ya wana yopitia wasanii wa muziki.

Akizungumza na ukurasa huu amesema mwaka umebadilika vizuri mashabiki zake wakae mkao wa burudani kwa kuwa anakuja kwa mtindo mpya.

“Nashukuru Mungu, nimeuona mwaka mpya mwaka huu nipo mbioni kutoa nyimbo ya tofauti na watu walivyo nizoea nina ngoma ya Bongo fleva ipo kwenye foleni mashabiki wa muziki wakae mkao wa burudani,” anasema Nagwa.

Aliongeza kuwa kutoa wimbo wa Bongo fleva haimaanishi kwamba ata acha kuimba singeli ila ni kutanua wigo wa sanaa yake na kuongeza mashabiki.

Nagwa ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri katika muziki wa singeli kwa mwaka 2021, kwa ngoma zake  Mshati, Mke wangu na Chawa aliyoshirikiana na Man Fongo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here