Home BUSINESS MKOA WA GEITA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUWASAKA WEZI WA MAHINDI...

MKOA WA GEITA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUWASAKA WEZI WA MAHINDI MASHAMBANI.


Na: Costantine James Geita.

Jeshi la polisi mkoani Geita limewataka wananchi wa mkoa huo Kutoa taarifakituo cha polisi pindi wanapoibiwa mahidi mashambani kwao baada ya kutokea wimbi kubwa la wizi wa mahindi ya kuchoma mashambani ndani ya mkoa huo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishina msaidizi Henry Mwaibambe amebainisha hayo wakati akizunguza na wandishi wa habari amewataka wananchi kutoa taarifa za wizi wa mahindi  mashambani ndani ya jeshi la polisi kwa lengo kusaidia jeshi hilo kukomesha tatizo  la wizi wa mahindi ya kuchoma mashambani katika maeneo mbalimbalii ndani ya mkoa huo

“Sisi tuna wito wetu kwa wakazi wa mkoa huu wa geita hatakama umeibiwa mahindi mawili ripoti kituo cha polosi wakiana mama wengi wanalalamika wameibiwa mahindi ya kuchoma sisi tumeanza ufuatiliaji wa tukio kama hilo lakini wangetusaidia zaidi wao kuleta taarifa” amesema  Henry Mwaibambe Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita.


Aidha mkurugenzi wa halmashauri ya  Geita mji pamoja na   John P Wamga Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Geita kwa pamoja wamekili uwepo wa tatizo hilo la wizi wa mahindi wamesema ili kumaliza tatizo hilo wananchi wametakiwa kushirikiana kwa pamoja kwa lengo la kutokomeza tatizo hilo.

“Swala hili sio tu la uongozi swala hili nilasisi sote kwetu sote ambapo hawa wezin hawatoki halmashauri ya mji hapa ofisini kwangu wanatoka hukohuko tunakao nao sisi na tunawafahamu kwahiyo ni swala la kuongeza ulinzi shirikishi na kushirikiana kwa pamoja ili tukomeshe hili swala’’ Amesema Zahara Michuzi mkurugenzi wa halmashauri ya  Geita mji.

“Kwenye wizi wa mahindi katika kijiji cha Buyagu na Mkolani maafisa watendaji wa kata na watendaji wa vijiji ni wenyeviti wa kamati ya  usalama ngazi ya kijiji kwahiyo tuwaombe muwajibike kuitisha vikao vya mara kwa mara na wananchi ili kuweka utaratibu wa ulinzi shirikishi katika maeneo yetu kwa sababu tukiwategemea polisi hawawezi kuwepo kila mahala” Amesema John P. Wan Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Geita.

Baadhi ya wakazi wa Geita wamelalamika na kusema kuwa swala hilo la wizi wa mahindi ya kuchoma mshambani limekuwa kama jambo la kawaida kutokana na matukio mbali mbali ya wizi wa mahindi kuwepo katika maeneo mbali mbali ya mkoa huo.

“Swala la wizi wa mahindi kwa ujumla kata ya nyankumbu kuendelea Buyagu limekuwa ni utamaduni wa kawaida watu wanalia kuibiwa mahindi shambani usiku na zinazofanya kazi kusomba ni piki piki “  mtu anaamka asubuhi anakuta shamba  limefyekwa zaidi ya nusu heka au hekali nzima ni lazima tupate majibu mazuri tumjue huyo mtu ni nani” Amesema Lukas Paulo Tito Mkazi wa geita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here