Home LOCAL MIRACOLO WASHEREHEKEA SIKU YA WAPENDANAO KWA KUWAFARIJI WAFUNGWA MAHABUSU

MIRACOLO WASHEREHEKEA SIKU YA WAPENDANAO KWA KUWAFARIJI WAFUNGWA MAHABUSU

NA: HERI SHAABAN, ILALA

Hospitali ya Miracolo iliyopo Tabata Sanene imetoa msaada wa magodoro, sabuni na pampasi katika Gereza la Segerea kama sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Wapendanao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Miracolo, Dk. Anna-pendo Deogratias, amesema waliguswa kutoa msaada huo ili kuwasambazia upendo watu wenye mahitaji wakiwemo wafungwa.

“Mbali ya kuwa na mpendwa wako uliyenaye karibu jaribu kufikiria na jamii nyingine, tuwasaidie wenzetu walioko kwenye mazingira magumu kwa kuwasambazia upendo,” amesema Dk. Anna.

Mkurugenzi huyo amesema pia katika kudumisha upendo kwa jamii inayowazunguka wanatoa huduma bure za uchunguzi wa afya ya kinywa na meno.

Kwa mujibu wa Dk. Anna huduma hiyo iliyoanza Februari Mosi itahitimishwa Februari 28 na kuwataka wananchi wajitokeze kuchunguzwa afya ya kinywa na meno.

Aidha amesema mpaka sasa watu wengi wamejitokeza kuchunguzwa ambapo wamebaini wengi wana matatizo ya kinywa na meno lakini hawajui.

Ameiasa jamii kutokimbilia kung’oa meno badala yake wafike kufanyiwa uchunguzi kwanza kwani mengine yanaweza yakatibiwa kwa kuzibwa.

Hospitali hiyo pia inatoa huduma mbalimbali za kibingwa ambapo kuna madaktari bingwa wa watoto, magonjwa ya ndani kama vile moyo, kisukari, presha, mfumo mzima wa chakula, magonjwa ya kina mama na vipimo vyote vya maabara.

Mwisho.

Previous articleSERIKALI YAWAJENGEA UWEZO WADAU JUU YA MKATABA WA AFCFTA JIJINI DAR
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.NNE FEBRUARI 15-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here