Home LOCAL MIAKA 55 YA AZIMIO LA ARUSHA WANANCHI, WAJASIRIAMALI WAKARIBISHWA KUONESHA BIDHAA ZAO,...

MIAKA 55 YA AZIMIO LA ARUSHA WANANCHI, WAJASIRIAMALI WAKARIBISHWA KUONESHA BIDHAA ZAO, SASA MABORESHO KUFANYIKA

 

Dkt Gwakisa Kamatula mkurugenzi wa makumbusho ya Azimio la Arusha  akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya miaka 55 ya Azimio la Arusha

 NA:NAMNYAK KIVUYO

Kuelekea kilele cha maadhimisho ya mipaka 55 ya Azimio la Arusha  yanayotarajiwa kufanyika Februari 4 wananchi wametakiwa kutembelea makumbusho ya Azimio hilo ili kuweza kujua historia na kujifunza  mambo mengi kuhusiana na nchi kwani makumbusho hayo sio kwaajili ya wazungu pekee.

Rai hiyo imetolewa na Dkt Gwakisa Kamatula mkurugenzi wa makumbusho ya Azimio la Arusha wakati akiongea na wandishi wa habari ambapo alisema kuwa watu wameanza kusau misingi iliyowekwa na waasisi wa nchi akiwemo baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere hivyo mwaka huu tukaona tuwe na wiki ya maadhimisho ambayo yameanza Februari 1 hadi 4.

“Lengo kubwa ni kujaribu kuwakumbusha watanzania kuhusu umuhimu wa misingi iliyowekwa katika Azimio la Arusha na watu wengi wanajiuliza kwanini imeitwa azimiao la Arusha lakini ni Azimio la Arusha kwamaana kwamba maadhimio, maamuzi ya nchi kuhusiana na sera za kufuata hasa baada ya uhuru yalifanyika hapa,” Alisema  Dkt Gwakisa.

Alifafanua kuwa ilibidi viongozi  wakae waamue ni jinsi gani wataiendesha nchi, ni sera gani wataifuata na ni misingi gani waiweke ili viongozi wa nchi na wananchi kwa ujumla waifuaye ili wote kwa ujumla waweze kwenda sawa hivyo iliwekwa misingi imara sana, misingi ya uongozi na misingi ya kulinda utaifa.

“Kwanza ni kulinda utaifa ambao nchi yetu ilikuwa imeshapita uhuru lakini kuhakikisha kwamba kunakuwa na haki na usawa kwa wananchi wote lakini pia walisisitiza kuwa nchi yetu ni masikini inabidi kila mmoja wetu aweze kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo binafsi na kuiletea nchi maendeleo kwa ujumla wake,” Alieleza.

Alieleza kuwa ni sera ambazo zilisaidi kuifikisha nchi hapa ilipo ikiwemo vita dhidi ya Rushwa, vita dhidi ya uonevu, matabaka na mambo mengine mengi hivyo lengo la maadhimisho haya ni kuendelea kuwakumbusha wananchi Kuna umuhimu wa kulinda uzalendo, uwajibikaji na kuweka mbele utaifa  kama ambavyo maadhimio yalivyotaka.

“Ni misingi ambayo bado inaishi  na sisi tufikiri ni vizuri kuwakumbusha wananchi hususan vijana ambao wanazaliwa leo wajue kuwa pamoja na kusoma katika vitabu wajue kwamba bado misingi Ile ipo na inafanya kazi lakini kama njia ya kudumisha misingi ya uwajibikaji na kujitegemea  tunawakaribisha wajasiriamali kuleta bidhaa zao Katika viwanja hivi vya makumbusho wauze kwasababu tunategemea kuwa na watu wengi,” Alifafanua.

“Waje wauze kazi zao, wajitangaze, tunao wasomi wengi mtaani  ambao badala ya kukaa tuu na kusubiri ajira ya serikali waje wajifunze hapa tutakuwa na mada kutoka kwa wataalamu mbalimbali kuhusiana na suala zima la namna ya kufanya ujasiriamali, kujitegemea kiuchumi lakini pia tutakuwa na mtaalamu kutoka time ya maadili ambaye Atakuja kutukumbusha kuhusiana na suala la uzalendo , utaifa na maadili ya mtu mmoja mmoja na hata viongozi,” Alisema Dkt Gwakisa.

Alisema sambamba na maadhimisho hayo siku ya kilele wanatarajia kuzindua mradi wa kuboresha makumbusho ya Azimio la Arusha ambapo serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu wamewapatia fedha  za kuweza kuifanya makumbusho hayo kuwa ya kisasa, kuweka maonesho ya kisasa, vifaa vya kiteknolojia yanayoendana na wakati ili wananchi au watalii wa ndani na nje watakao tembelea waweze kupata historia ya nchi kwa uzuri na kwa wepesi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here