Home LOCAL MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI NJOMBE YAPAMBA...

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI NJOMBE YAPAMBA MOTO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akisisitiza jambo kwa Viongiozi wa Mkoa wa Njombe na Kamati ya Mkoa alipofanya ziara ya kukagua Maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa Sabasaba. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Kasongwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto) akiwa ameongozana na Viongiozi wa Mkoa wa Njombe na Kamati ya Mkoa alipofanya ziara ya kukagua Maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa Sabasaba Februari 23, 2022. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Mhandisi Marwa Rubirya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akikagua sehemu ya ukoka katika uwanja wa Sabasaba alipotembelea kwa lengo la kukagua Maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Mhandisi Marwa Rubirya (kulia) akifafanua jambo wakati walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye UlemavU) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako walipotembelea uwanja wa Sabasaba kwa lengo la kukagua Maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akivalishwa Skafu na vijana wa Halaiki alipowatembelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mpechi.
Sehemu ya vijana wa Halaiki wakiwa katika mazoezi katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Mpechi kuelekea katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na vijana wa Halaiki alipowatembelea katika Shule ya Sekondari Mpechi kwa lengo la kukagua maandalizi ya mazoezi yao kuelekea katika uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari akitoa taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kukagua Maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU) OWM – KVAW
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amepongeza Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa hatua nzuri waliyofikia kuelekea katika uzinduzi wa tukio hilo muhimu linalotarajiwa kufanyika Aprili 2, 2022 Mkoani Njombe.
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati hiyo, Waziri Ndalichako alieleza kuridhishwa na hatua za awali za maandalizi na kuipongeza kamati ya Mkoa kwa kuendelea kusimamia na kuratibu vyema shughuli hiyo ya maandalizi.
Kwa namna maandalizi haya yanavyoendelea vizuri inadhihirisha kuwa tulifanya maamuzi sahihi kuteua Mkoa wa Njombe kuwa ni sehemu ambayo Mbio za Mwenge wa Uhuru zitazinduliwa,
Hongereni kwa maandalizi ambayo mmefanya mpaka sasa na niwapongeze kwa kuonyesha utayari wa kuhakikisha shughuli hii ya kitaifa inafana, maana maandalizi mazuri yataleta heshima kwa Mkoa huu, hivyo mzingatie masuala yote ya msingi yatakayofanya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Njombe una kuwa wa kihistoria,” alisema Waziri Ndalichako
Aliongeza kuwa, kila mwaka Mwenge wa Uhuru hukimbizwa katika Mikoa, Wilaya na Halmashauri zote nchini ikiwemo Bara na Visiwani.
Waziri Ndalichako alifafanua kuwa Serikali imepanga kufanya Sensa ya Wat una Makazi mwezi Agosti 2022, hivyo kauli mbiu ya Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022 ni; Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo; Shiriki Kuhesabiwa, Tuyafikie Maendeleo ya Taifa.
Sambamba na hayo Mheshimiwa Ndalichako aliwasihi wajumbe wa Kamati hiyo ya Mkoa kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao katika shughuli hiyo ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani humo.
Pia, Waziri Ndalichako alipokeza Mkoa kwa namna umekuwa ukishirikisha wadau ili waweze kujitokeza na kuchangia ufanikishaji wa shughuli hiyo ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Mhandisi Marwa Rubirya alisema kuwa Mkoa huo umejipanga vyema na maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru na aliahidi kusimamia shughuli zote za maandalizi kwa ufanisi na kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.
Nikuhakikishie uteuzi huu tutautendea haki na tutawezesha wananchi wa Mkoa wa Njombe wanashiriki katika tukio hilo muhimu na kutumia fursa hiyo ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kujitangaza kama Mkoa,” alisisitiza Mhe. Rubirya
Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alitembelea Uwanja wa Sabasaba ambapo uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kufanyika, pia aliwatembelea vijana wa Halaiki katika Shule ya Sekondari Mpechi Mkoani Njombe.
Previous articleABSA FINANCIAL MARKETS INDEX (AFMI 2021) LAUNCHED AS TANZANIA RECORDS SOLID PROGRESS IN KEY PILLARS
Next articleTRA GEITA YAWAONYA WAFANYABIASHARA MATUMIZI YA RISITI BANDIA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here