Home SPORTS KAMPUNI YA PEAKTIME MEDIA YADHAMIRIA KUENDELEZA VIPAJI VYA MCHEZO WA NGUMI JIJINI...

KAMPUNI YA PEAKTIME MEDIA YADHAMIRIA KUENDELEZA VIPAJI VYA MCHEZO WA NGUMI JIJINI DAR

Na: Stella Kessy, DAR.

KAMPUNI ya Mchezo wa Masumbwi Tanzania Peaktime Media imesema mashindano ya Ngumi kati ya Wilaya za Dar es salaam yanatarajia kufanyika ili kuendeleza Vipaji na kuibua wadau wa ngumi za kulipwa Nchini.

Mapambano hayo ya Kumsaka Nyota wa Mtaa(Champion wa kitaa) yanatarajiwa kufanyika Februari 20, 2022 katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Kauli hiyo imetolewa na mratibu Mkuu wa Peaktime Media Meja Selemani Semunyu wakati wa Kufungua Tamasha la Mapambano ya Kumtafuta Bondia Nyota wa Mtaa (Champion wa Kitaa) lenye lengo la kuendeleza ngumi nchini.

Ameongeza kuwa tamasha hilo la Champion wa Kitaa linalenga kukuza vipaji vya Masumbwi kwa mabondia wadogo mtaani ambao wamekua wakikosa Nafasi ya kuonyesha vipaji vyao ili hatimaye waipeperushe bendera ya Masumbwi ndani na Nje ya Tanzania.

Aidha Katika Uzinduzi wa Mapambano hayo Mabondia nguli Alphonce Mchumiatumbo na Alex Sitampini walitambiana Mbele ya Mashibiki huku wakiahidi kuonyesha kazi kwenye Pambano lao la Uzito wa Juu (Cuiser Weight Kg 91).

Mabondia waliofanya vizuri katika Uzinduzi wa Mapambano hayo ni Abdallah Muhumba wa keko, Omary Matimbwa dhidi ya Bakari kitogo wa Mbagala, David Edward dhidi ya Adam sega, Saidi Uwezo dhidi ya Saidi Mohamed, Enock Enock dhidi ya Said Ndilimo, Sebastiani Deo dhidi ya Amour Sheikh Hajj, Peter Tosh Dhidi ya Ramadhan Msham huku pambano la Jadi Salehe na Husein Mkalekwa wakitoka Sare na kupendekezwa pambano hilo lirudiwe Februari 27, katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here