NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa ya kulevya imetoa elimu kwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha, viongozi wa dini, madiwani na watendaji wa kata juu vita dhidi ya madawa hayo ili kwa pamoja waweze kushirikiana na kuhakikisha wanakuwa na Tanzania huru isiyokuwa na matumizi ya dawa ya kulevya.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Mkuu wa Arusha John Mongela alisema kuwa juhudi za serikali za kupambana na dawa za kulevya zinatakuwa ziungwe mkono na kila raia mzalendo kwani mzigo wa athari za dawa hizo unalifika taifa zima.
Mongela amewataka viongozi hao kuyachukua mafunzo hayo kwa umakini ili yakawe na manufaa katika kupambana na dawa za kulevya kwani serikali inatumia gharama kubwa kupambana na watu wanaotaka kuliharibu taifa lakini pia katika uwekezaji wa utoaji elimu hiyo.
“Baada ya mafunzo haya nendeni mkapige vita matumizi ya dawa ya kulevya ili kuhakikisha vijana wanabaki na akili timamu kwa mustakabali wa taifa kwani madawa yanayosafirishwa yapo kwa kiwango kikubwa hivyo mkawe mabalozi,” Alisema Mongela.
Kwa upande wake Kamishna Generali wa mamlaka hiyo Gerald Musabila Kusaya alisema kuwa wanachotaka ni kuhakikisha elimu inamfikia kila mtanzani ili waweze kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambapo hadi sasa watu wanaotibiwa kutokana na athari za dawa za kulevya ni 10,600.
“Tunachotaka ni taarifa juu ya watu wanasafirisha na kuuza madawa ya kulevya katika nchi yetu na kuvunja mtandao huo ili tuweze kumaliza suala hili na kuwa na Tanzania huru isiyokuwa na matumizi ya dawa za kulevya,” Alisema Kamishna Generali Kusaya.
Alieleza kuwa katika kipindi cha 2021 walikamata kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kilo 859.29 zilizoingizwa kutoka nchi za nje ambapo ni kiwango kikubwa cha madawa ya kulevya kukamatwa tangu nchi kupata uhuru ambapo mafanikio hayo yalisababishwa na watanzania wenye mapenzi mema na nchi yoa.
“Tukiendelea kupata ushirikiano mzuri tunaoupata kwa watanzania wote ni dhairi kwamba kila mmoja aliendelea kuchukia dawa za kulevya ni imani yangu hii vita tutaikamilisha ndani ya kipindi kifupi,”Alisema.
Alifafanua kuwa katika kipindi cha Januari 2021 Hadi hivi sasa wamekamata kilo 950.8 za dawa za kulevya kutoka nje ya nchi lakini pia kuangamiza mashamba ya bangi zaidi ya hekari 10.5 na kukamatwa zaidi kilo 860 za mirungu ambapo watuhumiwa zaidi ya 500 wamekamatwa
Naye Askofu Stanley Hotae wa kanisa la Anglikana alisema kuwa ni vema serikali ikaingiza somo la vita dhidi ya dawa ya kulevya shule za msingi ili watoto ambao ndio vijana wa kesho wakue wakijua dawa za kulenywa nini na athari zake ni zipi kuliko kuja kuangaika kutoa elimu wakati wakiwa tayari wameshapata madhara.