Home BUSINESS DC JOKATE AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WABADHIRIFU WA FEDHA ZA MIKOPO YA...

DC JOKATE AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KALI WABADHIRIFU WA FEDHA ZA MIKOPO YA ASILIMIA 10

Mkuu wa Wilaya Temeke Jokate Mwegelo (kushoto) akikabidhi ripoti maalum ya uchunguzi wa fedha za mikopo asilimia 10 kwa Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Temeke(katikati).Kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Sehemu ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya ya Temeke wamkifuatilia kwa makini Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo ( hayuko pichani) wakati akiizungumzia ripoti ya uchunguzi wa fedha za mikopo iliyokabidhiwa kwake na Kamati ya Usalama ya Wilaya

Na: Mwandishi wetu.

MKUU wa Wilaya ya Temeke amesikitishwa na madudu ambayo yamebainika kwenye ripoti maalum ya uchunguzi wa fedha ya mikopo aslimia 10 ambayo hutolewa na Halmashauri kwa ajili ya wanawake vijana na watu wenye ulemavu ambapo kutokana na hali hiyo ametoa maelekezo wote ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine katika ubadhirifu wa fedha hizo za mikopo wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Pia ametoa maelekezo ya kutaka Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halnashauri ya Temeke asimamishwe kazi kwa muda kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza kwenye ripoti hiyo ya uchunguzi maalumu iliyoandaliwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya.

Akizungumza wakati akipokea ripoti hiyo mbele ya viongozi wa Wilaya hiyo, watendaji wa Mitaa na Kata pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)kutoka wilaya hiyo, Jokate amesema hawezi kufumbia macho upotevu wa fedha za mikopo, hivyo ameagiza TAKUKURU na Polisi waendelee kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua haraka.

Akifafanua zaidi kuhusu ripoti hiyo amesema kuna vikundi vimepata mikopo lakini hakuna shughuli inayofanyika kwa maana waliomba kwa ajili ya shughuli fulani lakini hawaifanyi.”Tumeambiwa kuwa baadhi ya vikundi kupita ngazi ya Kata na mtaa na kisha inapitishwa na idara ya maedeleo ya jamii ngazi ya wilaya kwa maana havifuati utaratibu uliwekwa.

“Vikundi lazima vitambuliwe ngazi ya mtaa na kisha vipitishwe ngazi ya kata na baada ya hapo vithibitishwe ngazi za manispaa, pia wengi ambao wamepitiwa wamesema kumekuwa na mashinikizo, lakini tumepata changamoto kwa baadhi yetu viongozi kuwa sehemu ya vikundi vinavyopatiwa mikopo kadha kwa kadhaa kwa hiyo ni sehemu ya mapungufu.

“Kuna vikundi wamepewa mikopo muda mrefu na hawana shughuli waliyoifanya, huu ni upotevu wa fedha za umma , lakini unakuta kuna miradi imehamishwa kutoka sehemu za mwanzo iliyokaguliwa, kuna vikundi vimebadilishwa mradi walioandika awali maana yake hawakufuata utaratibu.Nilikuta live bila chenga kikundi kimepokea hela lakini tulipofika pale wanaulizwa maswali hawana majibu, tukaona hapa kuna ukakasi,”amesema Jokate.

Pia kuna vikundi ambavyo havina mikataba na hicho ni mojawapo ya kiashiria kuna uzembe katika usimamizi wa vikundi.” Nimesikitika sana kuna watumishi ambao wamenyanyasika kwasababu tu ya kusimamia haki, kuna watumishi wawili ikafika hatua wanataka kuhamishwa kwasababu tu wameamua kusimamia haki.Hatuwezi kukosa utu mbele ya watmishi wanaosimamia haki kuhakikisha wananchi wanapata haki inayostahili.

“Kumekuwa na changamoto katika utoaji mikopo na niliwaambia sisi ni viongozi wapya ndani ya wilaya hii ya Temeke ,mnakumbuka nimekuwa nikisisitiza hii dhamana niliyopewa na Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama chetu cha Mapinduzi Mama Samia Suluhu Hassan ni dhamana ambayo tumekula kiapo cha kuwatumikia wananchi.Pia dhamana ambayo inatutaka tuwatumikie wananchi kwa uadilifu.

“Lakini niwaleza nia yangu ni kuijenga Temeke yenye heshima, Temeke ya mfano , kwa hiyo naomba tujipongeze wote kwa kuwa mfano wa kufanya uchunguzi na kutoa ripoti hii.Kwa nafasi yangu nikiwa msimamizi mkuu wa shughuli zote za Serikali katika Wilaya ya Temeke niliamua kujihakikisha, kutokana na yale yaliyofanywa nyuma yasirejee katika utawala wetu.

“Mimi nataka nataka twende pamoja na ili twende pamoja lazima tuwe wawazi Majungu, fitna, chuki tuweke pembeni , kama viongozi lazima tuongee lugha moja ambayo ni kutawatumikia wana Temeke.Sasa kuna masuala hapa tumeyapokea kutoka kwenye taarifa na ni vema kila mtu ashike hamisini zake, kila mtu ashike majukumu yake.

“Utabebwa na uadilifu wako na miendendo yako, tusibebeshane lawama ambazo hatustahili kuzibeba, ndo maana tumetoa taarifa hii kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi, wote ambao wametajwa wachukuliwe hatua, kwenye maeneo ambayo manispaa inatakiwa kufanyia kazi basi yashughulikiwe, viongozi wenzangu hizi kazi ni za kupita, hizi kazi ni za utumishi, wengi tunapenda hizi nafasi zitutumikie badala sisi kutumikia nafasi zetu, tunajikosea sisi wenyewe, tunawakosea waliotupa dhamana.”

Ameongeza kwenye vikundi ambavyo wanakwenda kuvipa mikopo vipo takriban 119 na kati ya hivyo vikundi 21 wameshindwa kuvihakiki na hiyo inawapa kiashiria cha awali huenda havipo lakini thamani ya mkopo kwa vikundi hivyo 21 ni Sh.milioni 700.“Hiyo ni hela nyingi na sisi tulitoka wilaya za huko pembezoni hiyo bajeti ya nusu mwaka , hivyo hatutaki kurudia makosa yaliyotokea huko nyuma.Kwa hiyo vikundi ambavyo vinastahili mikopo watapewa mikopo na maelekezo yangu kwa halmashauri fedha za mikopo zianze kutolewa kwa wazi.”

Wakati huo huo amesema siku za karibuni kuna taarifa wamezipata kuna kiongozi alikuwa analobi ili Shule ya Sekondari Kurasini iuzwe na taarifa alizonazo Mkurugenzi wa Temeke alikuwa apewe Sh.milioni 100 lakini akakataa.”Nakupongeza Mkurugenzi maana sio rahisi kuona hela lakini umezikataa.Kama kuna tuna kiongozi mkubwa anateka kuuza shule ya sekondari.

“Tena ni miongoni mwa shule ambazo zimejengwa madarasa saba mapya kupitia fedha za Rais Samia Suluhu, mnataka kuiuza shule wanafunzi mnawapeleka wapi?Sisi viongozi mnatuacha wapi”Mwenzenu U-DC bado naupenda maana nataka kuendelea kuwatumikia wananchi,hebu tuongeeni ukweli, nabaki wapi mimi DC.Sasa leo hii Rais anatapa taarifa kuna mpango wa kuuza shule mnatuweka katika hali gani?”


 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here