Home LOCAL DC ARUSHA ATAKA ELIMU ITOLEWE KWA WANANCHI JUU YA ZOEZI LA ANWANI...

DC ARUSHA ATAKA ELIMU ITOLEWE KWA WANANCHI JUU YA ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI KUEPUKA WAFITINI WENYE NIA YA KUVURUGA ZOEZI HILO

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda akifungua mafunzo juu ya anwani za makazi iliyotolewa kwa wenyeviti  na watendaji wa mtaa jiji la Arusha.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima akiongea katika ufunguzi wa mafunzo ya anwani za makazi iliyotolewa kwa wenyeviti na watendaji wa mtaa na jiji hilo.

Baadhi ya wenyeviti na watendaji wa mtaa yote ya jiji la Arusha wakiwa katika mafunzo juu ya anwani za makazi

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Mkuu wa wilaya ya Arusha  Said Mtanda amewataka wenyeviti na watendaji wa mtaa kwenda kutoa kwa usahihi elimu waliyoipata katika mafunzo yao juu ya umuhimu wa anwani za makazi kwa jamii na nchi kwa ujumla ili kuepuka wafitini wenye mpango wa kupeleka uvumi usio wa kweli kwa nia ya kuvuruga zoezi Hilo.

Mtanda aliyasema hayo  wakati akifungua  mafunzo kwa wenyeviti na watendaji wa mitaa yote ya jiji la Arusha ambapo alisema kuwa wananchi wasipoelewa zoezi hilo vizuri wanaweza kutokea watu wenye fitina  wakanza kupotosha juu ya zoezi hilo lenye manufaa makubwa kwa jamii na nchi kwa ujumla.

“Kwa hiyo mmefanya vizuri kuwahusisha wadau waelewe umuhimu wa zoezi la makazi maana yake nini,lakini ni vyema mkafanya kazi kwa umoja na mshikamano ili iweze kukamilika kwa wakati hadi kufikia machi mwaka huu liwe limekamilika, “alisema Mtanda.

Aidha  aliipongeza halmashauri ya jiji la Arusha kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika mfumo wa zoezi la anwani za makazi  ambapo aliwasihi wenyeviti na watendaji hao wakafuata yale waliyoelekezwa kupitia mafunzo huu na kuacha kuanzisha utaratibu wao wenyewe ambao unaweza kuleta mitafaruko katika jamii hali ambayo inaweza kusababisha kutofika  muhafaka wa zoezi hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha,Dkt.John Pima alisema zoezi hilo limezindulia rasmi na Mkuu wa wilaya huyo Said Mtanda ikiwa kimkoa walizindua mnamo februari 22,2022 na Mkuu wa  mkoa wa Arusha,John Mongella.

Dkt.Pima alisema zipo baadhi ya kazi zimeshafanyika kwa lengo la kuandaa timu pamoja na zoezi la utoaji wa elimu ambapo watendaji na wenyeviti wa mtaa ndio watakaokwenda kuhitisha vikao vya kwanza katika utambuzi wa barabara kwenye maeneo yao

“Timu hii ndio ambayo inatakiwa iandike muhitasari na izingatie utaratibu wa kuleta majina hayo na namna ambazo nyumba zitapangwa  kwani ndio inayohusika na kufahamu maeneo yote, “alisema Dkt.Pima

Mkurugenzi huyo alisema kata ambazo wataanza nazo ni kaloleni, kati, Levolosi, Themi,  pamoja na sekei ifikapo februari 28 mwaka huu ziwe zimekamilika kwani hatua walizochukua hadi sasa ni kuandaa watendakazi na kata hizo zitaanza Februari 15, 2022 ikiwa taratibu zote zimeshakamilika na kata 20 zilizobaki zitaanza februari 21,2022 kutokana mchakato wa kutafuta watumishi wa muda wa zoezi hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here