Home SPORTS BEKI WA YANGA JOB APIGWA FAINI,AFUNGIWA MECHI TATU

BEKI WA YANGA JOB APIGWA FAINI,AFUNGIWA MECHI TATU

Na: mwandishi wetu

BEKI  wa Klabu ya Yanga, Dickson Job amefungiwa kuweza kucheza  mechi tatu kwa msimu wa 2021/22 na Kamati ya Bodi ya Ligi Tanzania ambayo imetoa taarifa hiyo leo Februari 11.

Mbali na kufungiwa kucheza mechi tatu za ushindani ambazo ni pamoja na zile za Kombe la Shirikisho pamoja na za ligi nyota huyo pia amepigwa faini ya laki tano.

Yote hayo imetokana na kosa la kumkanyaga mchezaji wa Mbeya City, Richardson Ng’ondya ambalo ni hatari kwa afya ya mchezaji ndani ya uwanja.

Job alifanya tukio hilo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Mkapa na ubao ulisoma Yanga 0-0 Mbeya City.

Baada ya tukio hilo Job aliweza kuomba msamaha kutokana na kufanya jambo hilo ambalo si la kiungwana kwa familia ya michezo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here