Home LOCAL BALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA ZIARA YA RAIS SAMIA...

BALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA ZIARA YA RAIS SAMIA UFARANSA

 

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui akizungumza na waandishi wa habari katika makazi yake Jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio ya ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya hivi karibuni nchini Ufaransa.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi hao Jijini Dar es Salaam. (kushoto) ni Afisa Habari wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Iku Kasege

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui (kulia) akizungmza na Maofisa na wafanyakazi wa Ubalozi huo wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru kwa kufanikisha maandalizi na safari ya Rais Samia na ujumbe wa Tanzania kwenda Ufaransa. (kshoto) ni Mke wa Balozi huyo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui amezungumzia mafanikio ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Ufaransa hivi karibuni ambayo imezaa matunda na kuleta mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Balozi Hajloui ameyasema hayo leo Februari 18,2022 alipozungumza na waandishi wa habari katika makazi yake Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa katika ziara hiyo Rais Samia alikutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na kupata fursa ya kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Aidha katika mazungumzo hayo kumekuwepo suala la kuboresha ulinzi na utunzaji wa bahari na kuhakikisha kunakuwepo mikakati madhubuti ya kuimarisha uchumi na kuangalia namna bora ya kufikia mafanikio katika uchumi wa bluu, pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji katika Majiji makubwa.

Amesema kuwa pia viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia mambo mengine yakiwemo uwekezaji wa biashara baina ya nchi hizo mbili na kuendelea kukuza Diplomasia.

”Tunampongeza Rais Samia kwa kufanya ziara katika nchi yetu ya Ufaransa kwani imekuwa na mafanikio makubwa, imefungua fursa mbalimbali za kiuchumi na kuleta mabadiliko  makubwa.” amesema Balozi Nabil

Akifafanua zaidi kuhusu ziara hiyo amesema anashukuru kuona Tanzania na Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD wameingia makubaliano na kutiliana saini mikataba mitatu ya miradi ya maendeleo yenye ufadhili wa jumla ya Euro milioni 259 na kwamba miradi hiyo itajikita katika sekta ya kilimo, uchukuzi na miundombinu, pamoja na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Tanzania.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha nchi hizo zinaendelea kukuza ushirikiano ulipo kutakuwa na ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa utakaokuja Tanzania kwa lengo la kukutana na mamlaka za biashara kwa lengo la kupanua wigo wa uwekezaji utakaokuza uchumi na maendeleo.

“Wafanyabiashara hao wakiwa hapa nchini pamoja na kukutana na viongozi wa kiserikali watakuwa na ratiba ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu.Wafanyabiara hao kutoka nchini Ufaransa wakiwa hapa Tanzania watakuwa na programu maalumu ya kuwainua wajasiriamali wachanga”amesema Balozi Nabil.

Hivi Karibni Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara nchini Ufaransa kuhudhuria kilele cha mkutano uliohusu rasilimali bahari (One Ocean Summit) uliofanyika Febrari 11,2022 katika Jiji la Brest nchini Ufaransa uliowakutanisha viongozi mbalimbali wa nchi zenye ukanda wa rasilimali bahari kufuatia mwaliko wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Katika hatua nyingine balozi huyo amekutana na kufanya mzungumza na Maofisa na watumishi wa  Ubalozi huo ambao wamekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha ujumbe wa serikali ya Tanzania uliombatana na Rais wa Tanzania kufanikisha ziara yake nchini ufaransa.

mwisho

PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO HILO.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here