Home LOCAL ASKOFU JACKSON KUONGOZA SEMINA YA UMOJA WA VIJANA ANGLIKANA NA MAOMBI KWA...

ASKOFU JACKSON KUONGOZA SEMINA YA UMOJA WA VIJANA ANGLIKANA NA MAOMBI KWA TAIFA

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Jackson Sosthenes anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Katika Semina maalum la Umoja wa vijana wa kanisa hilo ambapo pamoja na Mambo mengine imelenga kuliombea Taifa.

Kongamano hilo ambalo linatarajia kufanyika februali 5, 2022  Katika Kanisa la Mtakatifu Batolomayo lililopo Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es Salaam .ambapo pia makanisa yote ya Angalikana Dayosisi hiyo yatahudhuria.

kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo Vijana Dayosisi ya Dar es salaam John Kibata imesema lengo la kufanyika kwa semina hiyo na nikuliombea taifa na kuwaleta pamoja vijana wote kwa ajili ya kufungua mwaka mpya.

Pia imesema kuwa jambo lingine litakalojili  nikufanyika kwa maombi ya pamoja,kwa ajili ya taifa na kanisa kwa ujumla ikiwa ni kuwaleta pamoja Vijana hao.

Katika semina hiyo licha ya kuwa na matukio mbalimbali pia kutafanyika maombi maalum ,na semina maalum itakayoongozwa Askofu wa Dayosisi hiyo,na matukio mengine mbalimbali.

Pia katika taarifa hiyo Katika semina hiyo kwaya mbalimbali zitapata fursa ya kutuimba nyimbo zao hivyo waumini wote wa kanisa hilo wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo maalum.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here