Home SPORTS YANGA YAENDELEZA VICHAPO LIGI KUU

YANGA YAENDELEZA VICHAPO LIGI KUU


 Na: Stella Kessy.

KLABU ya Yanga leo imeichapa Polisi Tanzania bao katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha.

Katika dakika ya  kiungo mshambuliaji wa Yanga Dickson  Ambundo  aliweza kupachika bao hilo dakika ya 64 kwa pasi ya Fiston Mayele mbele ya Polisi Tanzania.

Yanga wanasepa na pointi tatu mazima mbele ya Polisi Tanzania na kuvunja mwiko wa kutushinda ugenini.

Metacha Mnata ametunguliwa bao hilo kipindi cha pili huku kipindi cha kwanza akiwa katika ubora kwa kuzuia mabao katika lango lake.

Yanga inafikisha pointi 35 ikiwa nafasi ya kwanza na haijapoteza mchezo ndani ya ligi huku Polisi Tanzania ikiaki na pointi 18 na zote zimecheza mechi 13.

Previous articleHAKUNA KIINGILIO MECHI YA TANZANITE Vs ETHIOPIA
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI J.TATU YA LEO JANUARI 24-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here