Home SPORTS YANGA SC YAENDELEZA UBABE, YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 TANGA

YANGA SC YAENDELEZA UBABE, YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 TANGA

Na: Mwandishi wetu, TANGA.

Klabu ya Yanga Sc imeendelea kujiimarisha Katika uongozi wa ligi ya Soka Tanzania Bara (NBC PREMIER LEAGUE) kwa kuendeleza vichapo kwa kuichapa bao 2-0 Coastal Union ya Tanga.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Dimba la Mkwakwani Jijini Tanga timu ya Yanga ilionekana kulishammbulia lango la Coastal Union na dakika 40 ya mchezo huo ilifanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji wake machachari Fiston Mayele akipiga kichwa kUfuatia krosi ilipigwa na Djuma Shaban.

Goli la pili la Yanga liliwekwa kimyani na Said Ntibazokiza dakika ya 90 ya mchezo akipokea pasi murua kutoka kwa Farid Mussa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here