Home SPORTS WAITARA TROPHY KUTIMUA VUMBI JANUARI 29,2022 DAR

WAITARA TROPHY KUTIMUA VUMBI JANUARI 29,2022 DAR



Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM

MASHINDANO  ya Johnnie Walker Waitara Trophy yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi  Januari 29 mwaka huu. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo,  Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo,Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, amesema lengo la kuandaa mashindano hayo ni heshima ya kuendelea kimuenzi  muasisi wa klabu  hiyo,Jenerali George Waitara ambayo hufanyika kila mwaka Novemba lakini 2021 halikifanyika hivyo linafanyika mwaka huu.

Alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha wachezaji  kutoka klabu zote za hapa nchini kama vile Moshi klabu, Arusha Gymkhana, Mufindi klabu,Morogoro Gymkhana,Dar es Salaam Gymkhana,Sea cliff golf klabu Zanzibar, Kili Golf na TPC Golf klabu.

Aliongeza kuwa mwitiko wa wachezaji ambao watakaoshiriki ni mkubwa kwani Mpaka sasa wachezaji ambao wamesajiliwa kushiriki ni 100 na bado usajili unaendelea mpaka Alhamisi asubuhi ndio itakuwa mwisho wa kusajiliwa.

“Maandalizi yanakwenda vizuri tuna uwezo wa kupokea idadi ya wachezaji wowote, watu waendelee kujisajili,” amesema.

Aidha alisema nafasi ya watoto haitakuwepo kwa  sababu ya wadhamini wao  ni wa kileo hivyo ni kinyume na malezi ya watoto.

Kwa upande wake nahodha wa klabu hiyo, Meja Japhet Masai, alisemakuwa mashindano hayo ni ya siku moja ambapo itaanza na shindano la  wachezaji wa kulipwa ambao watacheza siku ya Ijumaa.

Alisema wachezaji  wa ridhaa kwa maana ya Div A,B,C, Seniors,na Ladies watacheza siku ya Jumamosi Januari 29. 

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti, Lumuli Minga ambao ni wadhamini wa mashindano hayo, alisema ni jambo la furaha kwao kuendelea kutengeneza fursa mbalimbali.

“Katika hili shindano la Waitara Cup tupo kwa miaka mitatu na tutaendelea kuwa wadhamini, dhamira ni kuendeleza gofu nchini,” alisema Lumuli.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here