Home BUSINESS TANZANIA NA MISRI ZAKUBALIANA USHIRIKIANO KATIKA KUIMARISHA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO,...

TANZANIA NA MISRI ZAKUBALIANA USHIRIKIANO KATIKA KUIMARISHA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO, USAFIRI, MIUNDOMBINU YA UMEME, MAJI NA USAFIRI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. balozi Mohamed Gaber Abulwafa na kujadiliana masuala mbalimbali ya Uwekezaji na fursa mbalimbali zilizopo baina ya nchi hizi mbili.

Mhe. Dkt. Kijaji amesema kuwa uhusiano na ushirikiano wa Uwekezaji baina ya Misri na Tanzania umekuwa ukiimarika zaidi baada ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya tarehe 10 Novemba, 2021 kukutana na Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.

Mhe. Dkt. Kijaji ameeleza kuwa fursa za biashara na uwekezaji kati ya Misri na Tanzania ambapo kwa hivi sasa biashara baina ya nchi hizo mbili imeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 84.3 mwaka 2018 hadi kufikia Shilingi Bilioni 87.3 mwaka 2020 hivyo kuna kila sababu yakuendeleza majadiliano na makongamano ya biashara baina ya nchi hizi mbili ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutumia fursa za uwekezaji.

Naye balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Balozi Mohamed Gaber Abulwafa amesema kuwa Nchi ya Misri imewekeza nchini Tanzania katika miradi 26 yenye thamani ya kiasi cha Shilingi Trilioni 3.1 na kutengeneza ajira 2,206 kwa watanzania.

Mhe. Balozi Mohamed Gaber Abulwafa amesema kuwa wawekezaji kutoka Misri walishafika nchini Tanzania katika Kongamano la Biashara lililofanyika nchini Tanzania ambapo wafanyabiashara wa Misri walipata fursa mbalimbali za kuwekeza na sasa wanaendelea na taratibu mbalimbali kuja kuwekeza Tanzania katika sekta ya Kilimo na Mifugo hasa biashara ya korosho, parachichi na Mahindi.

Aidha ameongeza kuwa Misri wapo katika hatua za ukamilishwaji wa kuanza kwa usafiri wa abiria kwa njia maji marine transport kutoka Misri hadi Tanzania ili kukuza Uwekzaji na Biashara na kurahisha usafirisjhaji wa bidhaa katika nchi hizi mbili.

Mhe. Dkt. Kijaji amemalizia kwa kusema kuwa Nchi ya Misri imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati katika nchi ya Tanzania ukiwemo ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) unaotarajiwa kukamilika Mwezi Juni 2022 na kusaidia Viwanda vyetu kuzalisha kwa uhakika kwani changamoto ya umeme nchini itakuwa imekwisha.

                                              

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here