Home BUSINESS STAMICO YAZIDI KUPAA HATIMAYE MGODI WA CHINI (UNDERGROUND MINE) -KIWIRA UPO TAYARI...

STAMICO YAZIDI KUPAA HATIMAYE MGODI WA CHINI (UNDERGROUND MINE) -KIWIRA UPO TAYARI KWA UZALISHAJI.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse tarehe 29 Januari 2022 pamoja na viongozi wengine wa STAMICO wamepata fursa ya kujionea ukarabati mkubwa wa miundombinu  ya mgodi wa chini (underground mine) katika Mgodi wa Kiwira kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe na kuhudumia wateja wengi zaidi. (massive coal mining)

Katika ziara hiyo Dk. Mwasse alipata maelezo na ufafanuzi wa ukarabati mbalimbali uliofanyika kutoka kwa mratibu wa mradi huo Mhandisi Peter Maha ambaye alieleza mafanikio ya hatua mbalimbali zilizofanyika  katika kukarabati Mgodi huo ikiwa ni kurejesha njia za reli,Mifumo ya hewa,maji na umeme na matengenezo ya mikanda ya kusafirishia makaa kuja nje ya mgodi ambapo makadirio ya uzalishaji wa makaa kwa mwezi ni tani 5,000.Aidha hadi sasa ukarabati wa miundombinu wa mgodi umefikia asilimia 98 na kuwa tayari kwa uzalishaji

Baada ya kutembelea mgodi huo wa chini Kaimu Mkurugenzi Mtendaji alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya na hatua zilizofikiwa katika ukarabati wa mgodi huo. Vilevile aliwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ilikuweza kufikia malengo ya makusanyo yaliyowekwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022

Kwa upande wao Watumishi wamemshukuru Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa kuweza kuwatembelea na kuongea nao kuhusu mipango hiyo ya Shirika. Ambapo kwa upande wao wamemuahidi kuongeza juhudi katika kuchapa kazi ili malengo mbalimbali  ya Shirika iliyojiwekea yaweze kufikiwa.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here