Home SPORTS SIMBA YATUA KAITABA KUIKABILI KAGERA SUGAR LEO

SIMBA YATUA KAITABA KUIKABILI KAGERA SUGAR LEO


Na: stella Kessy

KIKOSI cha Simba tayari kimewasili mkoani kagera kwaajili ya mchezo wa ligi Kuu ya NBC dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mchezo utakaochezwa katika dimba la kaitaba.


Kikosi kiliondoka jana kikiwa kamili kwa ajili ya mchezo huo ambao ni muhimu kwa timu hiyo ambayo malengo yake ni kupata alama 3.


Kikosi hicho ambacho hakijapata ushindi katika mechi mbili zilizopita lakini bado morali ya wachezaji ipo juu na wamehaidi kijitoa ili kuhakikisha wanapata ushindi.


Hata hivyo wachezaji wa kikosi hicho tayari wamefanya mazoezi ya kutosha  jana jioni na leo watafanya katika dimba la kaitaba kabla ya kushuka dimbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here