Home SPORTS SIMBA YAENDA NUSU FAINALI IKITOKA SARE YA 0-0 NA MLANDEGE FC

SIMBA YAENDA NUSU FAINALI IKITOKA SARE YA 0-0 NA MLANDEGE FC

Na: stella Kessy.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania Bara Simba leo wametoshana  nguvu  bila kufungana na Mlandege FC kwenye mchezo wa pili wa Kombe la Mapinduzi.
Dakika 90 zimekamilika kwa ubao wa Uwanja wa Amaan kusoma Simba 0-0 Mlandenge FC.
Licha ya Simba kuanza na wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na kipa namba moja Aishi Manula, mshambuliaji wao kibu Dennis pamoja na kiungo Pape Sakho ngoma ilikuwa ni nzito kwao.
Licha yakugawana pointi mojamoja wanafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kuwa wana jumla ya pointi nne kibindoni na mabao yao ni mawili.
Mchezo wao ujao wa nusu fainali unatarajiwa kuchezwa dhidi ya Namungo FC.

Previous articleRAIS MHE,.DK.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA MADARASA MAPYA SITA YA SKULI YA MSINGI SEBLENI
Next articleBITEKO AKEMEA MIGOGORO MAENEO YA WACHIMBAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here