Home SPORTS SIMBA, AZAM KUCHEZA FAINALI MAPINDUZI CUP

SIMBA, AZAM KUCHEZA FAINALI MAPINDUZI CUP

Na: Stella Kessy

KIKOSI cha Simba leo kimeibuka na ushindi wa bao 2-0  dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan katika Kombe la Mapinduzi unawafanya waweze kutinga hatua ya fainali.

Katika dakika za 14 Meddie Kagere  na PapeSakho dakika ya 48 yametosha kuwapa ushindi Simba.

Sasa Simba itakutana na Azam FC kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi Januari 13.

Azam FC ilishinda kwenye mchezo wa fainali ya kwanza dhidi ya Yanga na ilishinda kwa penalti 9-8.

Mchezaji bora wa mchezo wa leo amechaguliwa kuwa Sakho na amekabidhiwa zawadi ya milioni moja.

Frank Mangingi wa Namungo yeye amekabidhiwa tuzo ya mchezaji muungwana na amekabidhiwa laki tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here