Home BUSINESS SERIKALI IMEDHAMIRIA KUIFUFUA MIRADI YOTE YA NHC: NAIBU WAZIRI RIDHIWAN KIKWETE.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUIFUFUA MIRADI YOTE YA NHC: NAIBU WAZIRI RIDHIWAN KIKWETE.


Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwan Kikwete (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa NHC Dkt. Maulid Banyani (wa kwanza kushoto) wakangalia jengo la Morocco Square wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea mradi huo kujionea maendeleo yake.
Muonekano wa Jengo jipya la NHC la Morocco Square lililopo kwenye makutano ya Barabara ya Mwai Kibaki na Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwan Kikwete (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa NHC Dkt. Maulid Banyani (kushoto) wakiangalia muonekano mzuri wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa Katika moja ya jengo hilo ghorofa ya 8.

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwan Kikwete (wa kwanza kushoto) akiwa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo wakimsikiliza msimamizi wa jengo hilo alipokuwa akitoa Maelezo ya ujenzi wa mradi huo.

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwan Kikwete akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mara alipotembelea Ofisi za Shirika hilo leo Januari 24,2022 Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwan Kikwete akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za NHC Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Sophia Kongera (wa kwanza kulia) akiwa na wajumbe wa Bodi wa Shirika hilo Charles Silingi (katikati), na Abdullah Mwinyimvua ( (kushoto).

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwan Kikwete alipotembelea Shirika hilo. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Serikali imesema kuwa imedhamiria kuifufua miradi yote inayosimamiwa na kutekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) iliyokuwa imesimama.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Ridhiwan Kikwete amayasema hayo leo Januari 24,2022 Jijini Dar es Salaam alipotembelea Mradi wa ujenzi wa jengo la Biashara na Makazi la Morocco Square lililopo kwenye makutano ya Barabara ya Mwai Kibaki na Ali Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Kikwete amesema kuwa Serikali inatarajia kutoa fedha za kumalizia mradi huo kiasi cha Shilingi Billion 25.7 muda wowote kuanzia Sasa nakwamba ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 6 mara tu  ujenzi utakapoanza.

“Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa ya NHC katika Jiji la Dar es Salaam, binafsi yangu niseme nimeridhika na kazi niliyoiona, changamoto nilizoziona hapa ni katika kujua namna gani ya kumalizia mradi huu, kutafuta pesa ya kukamilisha  mradi huu” amesema Mhes. Kikwete.

Na kuongeza kuwa “Mradi huu umefikia 93% na tayari tumeshaomba fedha, hivyo tunasubiri sasa wenzetu wa Wizara ya Fedha kuweza kutupatia fedha iliyosalia kiasi cha Shilingi Billioni 25.7 kwaajili ya kukamilisha mradi huu” ameongeza.

Aidha amesema kuwa lengo la ziara yake kwenye shirika hilo ni kufahamu shughuli za Shirika hilo na kufanya mazumzo  ya kina na kujua kama kuna mikwamo yoyote ya kazi na mifumo yao pamoja na miradi yao kwa ujumla.

Kwà upande wake Mkurugenzi wa NHC Dkt. Maulid Banyani amesema kuwa mradi huo wenye majengo 4 yatakuwa na maeneo ya Biashara pamoja na eneo la makazi ikiwemo Hoteli, Maduka Makubwa, Kumbi za Sinema, Migahawa ya Chakula  na maeneo mengine ya Biashara.

“Mradi huu ukikamilika utatoa fursa nyingi za ajira kutokana na uwekezaji wa shughuli za Biashara zinazofanyika kwenye majengo haya, pia kwa upande wa makazi zipo nyumba zitakazouzwa na sehemu kupanishwa” amesema Dkt. Banyani.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo Dk. Sophia Kongera amemshukuru Naibu Waziri Kikwete kutembelea mradi huo na kujionea changamoto mbalimbali zinazoikabili mradi yao ukiwemo wa Morocco Square.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here