Home SPORTS RWEYEMAMU: TUMEJIPANGA KUFANYA VIZURI MAPINDUZI

RWEYEMAMU: TUMEJIPANGA KUFANYA VIZURI MAPINDUZI

 .

N:a Stella Kessy

MENEJA wa klabu ya Simba Patrick Rweyemamu amesema tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika michuano ya kombe la Mapinduzi nakwamba  hawataidharau timu yoyote kwani mechi zote zitakuwa kama fainali.

Rweyemamu amesema kuwa sababu ya kupeleka kikosi kizima ni kuhakikisha wanatimiza malengo ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kupita muda mrefu.

Akizungumzia mchezo wa kesho dhidi ya Selem View, Rweyemamu amesema wanaamini utakuwa mgumu na wapo tayari kupambana kwa ajili ya kupata alama zote.

“Tumekuja Zanzibar na kikosi cha wachezaji 26 tuliosajili msimu huu, kuna wengine wawili wamekuja kwa majaribio kwa hiyo wapo 28,hii inaonyesha wazi tumeshamilia kufanya vizuri” amesema.

Aliongeza kuwa katika kikosi cha wachezaji 28 ukiondoa wawili Taddei Lwanga na Erasto Nyoni ambao hawatakuwa sehem ya mchezo sababu bado wapo chini ya uangalizi wa daktari lakini waliobaki wapo kamili kupigania alama tatu.

Kwa upande wa mlinzi wa kushoto Gadiel Michael amesema morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo wa kesho lengo ni kupata ushidnj kwenye mechi ya ufunguzi.

“Wachezaji wote tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, kila atakayepata nafasi ya kucheza atapambana kuhakikisha wanapata ushindi”amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here