DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko Madogo katika Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu.
Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais Samia amefanya mabadiliko ya muundo katika Wizara tatu.
Mawaziri wapya watano walioteuliwa ni Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), Dk Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu), Anjelina Mabula (Ardhi) na Husein Bashe (Kilimo).
Rais Samia pia ameteua manaibu waziri wapya katika wizara tano.
Manaibu waziri hao wapya walioteuliwa ni pamoja na Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt. Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).
Tazama Video Hapa.👇👇👇👇
Baraza la Mawaziri.
Ofisi ya Rais Ikulu
Waziri wa Nchi Kazi Maalum – Kapeni Geroge Mkuchika
Waziri wa Utumishi – Jenista Mhagama
Naibu Waziri Utumishi – Deogratius John Ndejembi
TAMISEMI
Waziri – Innocent Bashungwa
Naibu Waziri – David Silinde
Naibu Waziri – Dugange
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Waziri – Suleimani Jafo
Naibu Waziri – Hamis Hamis
Wizara ya Kazi Ajira
Waziri – Ndalichako
Naibu Waziri – Patrobas Katambi
Wizara ya Fedha
Waziri – Mwigulu Mwigulu
Naibu Waziri – Chande
Wizara ya Ulinzi
Waziri – Stergomena Tax
Wizara ya Sheria na Katiba
Waziri – George Simbachawene
Naibu Waziri – Godfrey Mizengo Mizengo Pinda
Wizara ya Kilimo
Waziri – Hussein Bashe
Naibu Waziri – Anthony Mavunde
Wizara ya Uvuvi
Waziri – Mashimba Ndaki
Naibu Waziri – Abdallah Hamisi Ulega
Wizara ya Ardhi
Waziri – Angelina Mabula
Naibu Waziri – Ridhiwani Kikwete