Home SPORTS PETER BANDA AONDOKA KUUNGANA NA TIMU YAKE YA TAIFA AFCON

PETER BANDA AONDOKA KUUNGANA NA TIMU YAKE YA TAIFA AFCON

 

Na: Stella Kessy.

Winga  peter banda ameondoka leo kuelekea Malawi kwa ajili ya  kujiandaa na michuano ya Afcon  inayofanyika nchini Cameroon kuanzia january 9.

Banda amekwenda moja kwa moja Cameroon ambapo atakutana na Wachezaji wenzake tayari kwa Mashindano hayo.

Hata hivyo Malawi imepangwa kundi B pamoja na timu Senegal, Zimbabwe na Guinea, the flames itaanza kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya Guinea januari 10.

Banda amefurahi kushiri katika michuano hiyo kwa kuwa atakutana na Wachezaji wakubwa wanaofanya vizuri barani Ulaya ambapo atajifunza mengi kutoka kwao.

Ameongeza kuwa atahakiksha anafanya vizuri ili kulisaidia taifa  lake na kuitangaza Simba kupitia michuani hiyo mikubwa barani Afrika. 

“Hii ni michuano mikubwa na kila mchezaji afrika anatamani kushiriki kwangu ni jambo kubwa na nitahakikisha nafanya vizuri kuisaidia nchi yangu na kuitangaza Simba “amesema.

Banda atakutana na nyota wengine watatu wanaocheza ligi kuu ya NBC ambao ni Prince Dube, Bruce Kangwa, na Never Tigere wa Zimbambwa alio nao kundi moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here