Home SPORTS PABLO APIGWA FAINI YA MILIONI 2

PABLO APIGWA FAINI YA MILIONI 2

Na: Stella KESSY.

Na; Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KOCHA Mspaniola wa Simba SC, Pablo Franco Martin ametozwa faini ya Sh. Milioni 2 jumla kwa makosa mawili yanayofanana na kufungiwa mechi tatu kwa kupiga chupa chini kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Taarifa ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imesema kwamba Pablo ametozwa faini ya Sh. Milioni 1 kila mchezo dhidi ya Mtibwa na dhidi ya Kagera Sugar kwa kukataa kufanyiwa mahojiano na Waandishi wa Habari baada ya mechi hizo za ugenini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here