Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AZINDUA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UVIKO 19 KWA...

NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AZINDUA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UVIKO 19 KWA WATOA HUDUMA ZA UTALII DAR

Na: Hughes Dugilo, DAR.

Wizara ya Maliasili na Utalii imezindua Mafunzo kwa watoa huduma za Utalii Nchini kuhusu Mwongozo wa kukabiliana na janga la Uviko 19 katika Sekta ya Utalii yaliyoanza rasmi leo katika chuo cha Utalii Januari 29, Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii  Mary Masanja amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa katika Mikoa 26 nchini na yamelenga kuwafikia takribani watoa huduma 3900 katika Sekta ya Utalii.


Ameongeza kuwa ni wazi kwamba Utalii ni Sekta mtambuka na hivyo mnyororo wake wa huduma unahusisha wadau wengi.


Kwa kuzingatia na kutambua hali hiyo mafunzo hayo yatahusisha watoa huduma mbalimbali wakiwemo, watoa huduma katika tasnia ya Ukarimu na Huduma za makazi na chakula kama vile katika Hoteli, Loji na Kambi za kitalii.


“Pia aina mbalimbali za waongoza watalii, watoa huduma katika kupanda Mlima, uwindaji wa kitalii na utalii wa utamaduni, Wakala wa safari za kitali, Wakala wa usafiri wa anga, na wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wanahusika na kutoa huduma” amesema Masanja.


Aidha amesema wakati wa mafunzo hayo wadau hao watapata Elimu kuhusu Chanjo ya UVIKO 19 na pia kupata fursa ya kupatiwa Chanjo kwa wale walio tayari. 


“Niimani yangu kuwa juhudi hizi za Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwepo Sekta binafsi zinaleta tija na manufaa ya Utalii nchini kama ambavo imetiliwa mkazi Katika sera ya Taifa ya Utalii ya 1999 Katika kushirikiana kutatua changamoto, uendelezaji wa mazao ya Utalii na kutoa huduma Bora kukidhi mahitaji ya soko la Utalii” ameongeza.


Hata hivyo ameeleza janga la UVIKO 19 limeathili kwa kiasi kikubwa Sekta ya Utalii Duniani zikiwemo nchi ambazo ni masoko makuu ya Utalii, kwa upande wa Tanzania idadi ya watalii waliotembelea nchini ilipungia kutoka 152,7230 mwaka 2019 hadi 620,867 2020 sawa na upungufu wa asilimia 59.3.


Wakati mapato yatokanayo na Utalii yalipungua kutoka Dola za Marekani Billioni 2.6 mwaka 2019 hadi Dola za Marekani Billioni 0.715 mwaka 2020 sawa na upungufu wa asilimia 72.5.


Aidha amefafanua kuwa Sekta ya Utalii imeanza kuimarika kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahili wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuanzisha na kutekeleza mpango wa Taifa wa kukabiliana na janga la UVIKO 19.


Kwa upande wake mmoja wa wadau wa Sekta ya Utalii ambaye ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo Leina Lemomo kutoka Kampuni ya Utalii ya Nje Bush Camp and Msafiri Travels amesema mafunzo hayo yatawasaidi katika kuwajengea uelewa kuhusu janga la UVIKO 19, hivyo wataweza kujilinda wao wenyewe na kuwalinda wengine.


Aidha amesema janga la COVID 19 lilisababisha Utalii kufifia kwani kuna miaka miwili hakukuwa na kazi kabisa.


“Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuwa karibu na Dunia na mafunzo tunayopatiwa ni sehemu ya kuonesha kwa vitendo jitihada hizo” amesema.


MWISHO.

Previous articleRC MAKALLA AFURAHISHWA NA MWITIKIO MZURI WA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA ZOEZI LA USAFI WA PAMOJA
Next articleDC JOKATE MWEGELEO AZINDUA RASMI TUZO ZA WAJASIRIAMALI WA TWCC JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here