Home BUSINESS MOTO WAUNGUZA MADUKA 16 SOKO LA CCM KAKUBILO GEITA.

MOTO WAUNGUZA MADUKA 16 SOKO LA CCM KAKUBILO GEITA.



Na: Mwandishi wetu, GEITA.

Maduka 16 ya Wafanyabiashara wa soko la CCM kakubilo lililopo Wilaya ya Geita Mkoani Geita yameungua  na kuteketea kwa moto ambao hadi sasa bado chanzo  cha moto huo hakijajulikana.

Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya  ya Geita ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Geita,  Mhe.Wilsoni Shimo imefika katika eneo hilo na kujionea jinsi maduka hayo yalivyoteketea kwa moto halisi huku baadhi ya vitu kuibiwa na watu wasio julikana.

Hata hivyo  Shimo ameliagiza Jeshi la polisi kwa kushirikiana na uongozi wa soko hilo pamoja na Viongozi wa kata kuahakikisha wanashirikiana kuwasaka wote waliokwenda kutoa msaada na kuiba mali ambazo zilikuwa hazijateketea kwa moto

“Mwenzio alitarajia umekuja kuchukua zile nguo ambazo hazijaungua moto uzitunze mahala uumpe lakini wewe zile nguo unachukua unapeleka unakojua wewe mwenyewe huo ni wizi tabia hii na hii roho sio nzuri sana si jambo jema na huo si utanzania wetu ni bora hii tabia ikafichuliwa” Wilson Shimo mkuu wa wilaya ya Geita

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here