Home SPORTS MBEYA CITY YAICHAPA SIMBA SC 1-0 DIMBA LA SOKOINE

MBEYA CITY YAICHAPA SIMBA SC 1-0 DIMBA LA SOKOINE

Na: Mwandishi wetu, MBEYA.

Timu ya Mbeya City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao timu ya Simba SC ya Jijini Dar es Salaam.


Katika mchezo huo uliopigwa katika Dimba la Sokoine ambapo mshambuliaji Paul Nonga aliiongoza timu yake kwa bao la utangulizi katika dakika 19 bao lililolala kwa dakika zote 90 za mchezo huo.


Katika dakika ya 43 mlinzi wa upande wa kushoto wa Mbeya City ambaye ni Nahodha wa timu hiyo Mpoki Mwakinyuki alizawadiwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Simba Criss Mugalu.


kufuatia mchezo huo timu ya Mbeya City inaendelea kubaki katika nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya alama 22, ambapo Simba nayo inaendelea kushikilia nafasi ya pili ikibaki na alama zake 24.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here