Na: Stella Kessy, DSM
Kikosi cha wachezaji 24, viongozi na Benchi la ufundi wa timu ya soka KMC wameondoka Jijini Dr es salaam leo Januari 13 kuelekea Mkoani Rukwa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa siku ya Jumapili Januari 16 katika uwanja wa Nelsom Mandela Mkoani humo.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana imeendelea vema kujiimarisha kwa ajili ya mchezo huo ambapo katika safari hiyo licha ya kuwa na mechi dhidi ya Tanzania Prisons lakini pia KMC itakuwa na mchezo mwingine wa ugenini dhidi ya Mbeya kwanza Januari 21 mwaka huu katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mkoani Mbeya.
Akizungumza Ofisa Habari na Mawasiliano wa KMC Christina Mwagala amesema kuwa kikosi kimejiandaa vema na michezo hiyo ikiwa na kocha Mkuu Hitimana tangu alipotambulishwa rasmi Januari 6 mwaka huu akichukua mikoba ya aliyekuwa kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo na kwamba maandalizi hayo yanakwenda vizuri.
“Tunaenda kucheza mechi mbili ugenini ambazo kimsingi zitakuwa ngumu, tunakocha Mkuu mwingine ambaye ameanza kukinoakikosi hicho hivi karibuni, vivyo katika maandalizi yetu kikubwa tunachokihitaji ni kupata matokeo mazuri na kwmaba tunakwenda kupambania alama hizo sita muhimu kwani zipo ndani ya wetu”amesema
Aidha amesema kwa upande wa hali za wachezaji ni nzuri kwani wana morali kubwa ambayo kimsingi inajenga hari ya kwenda kupambana katika michezo ili kupata matokeo mazuri ikiwa ni katika mapambano ya mkakati wa kujiimarisha katika msimamo wa Ligi kuu ya NBC kwa maana ya kutoka kwenye nafasi ya 12 iliyopo kwa sasa na kupanda kwenye nafasi nzuri za juu.
“Timu zote ambazo tunakwenda kucheza nazo ni ngumu, na zinaushindani mkubwa, na siku zote mechi za ugenini zinakuwaga na ushindani mkubwa, hivyo tunakwenda kupambana kwa hali na mali kwani KMC ni Timu kubwa na yenye wachezaji wenye uwezo wa kupambana kwa ajili ya maslahi ya Timu” ameongeza