Home BUSINESS DKT. KIJAJI AKUTANA NA WAWEKEZAJI, WAMILIKI WA VIWANDA JIJINI DAR

DKT. KIJAJI AKUTANA NA WAWEKEZAJI, WAMILIKI WA VIWANDA JIJINI DAR


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt, Ashatu Kijaji, amekutana na wawekezaji, na wamiliki wa viwanda mbalimbali  na kujadiili changamoto wanazokabiliana nazo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini na kujenga uchumi shindani na viwanda. 

Katika mikutano hiyo, Waziri Kijaji amekutana na Viongozi wa Kampuni ya Dangote Tanzania inayozalisha Saruji, Kampuni ya Coca – Cola Kwanza ltd inayozalisha bidhaa mbalimbali za vinywaji baridi na Wawekezaji wa Kampuni ya Gynile kutoka Misri inayotarajia kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mbolea nchini. 

Wakati huo huo, Waziri Kijaji amekutana na baadhi ya Watendaji na  Wakuu wa Tume ya Ushindani (FFC), Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB ) na  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na  Biashara kujadili utekelezaji wa  majukumu ya Taasisi hizo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kuleta maendeleo kwa taifa.

Aidha  Waziri Dkt. kijaji amezitaka taasisi zote chini ya Wizara Uwekezaji Viwanda na Biashara kufanya kazi kwa ushirikikiano na kuepuka kuwa kikwazo kwa wawekezaji, wenye viwanda na wafanyabiashara  ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ili kuendeleza na kukuza sekta ya uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Previous articleWAZIRI BASHUNGWA AMPONGEZA MKURUGENZI WA DART DK.EDWIN MHEDE KWA KUONGEZA MAPATO
Next articleKAMATI ZA UKIMWI ZAAGIZWA KUKUTANA NA KUSHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here