Home LOCAL DKT. CHAULA AKABIDHIWA OFISI RASMI NA DKT JINGU

DKT. CHAULA AKABIDHIWA OFISI RASMI NA DKT JINGU


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Zainabu Chaula akikabidhiwa nyaraka za Wizara kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Zainabu Chaula akizungumza katika makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza katika makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza katika makabidhiano ya Ofisi kati ya Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu ambaye sasa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainabu Chaula katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM

Na: WMJJWM Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainabu Chaula amekabidhiwa rasmi Ofisi ya Wizara na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii ambaye kwasasa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. John Jingu.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  kuiunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Katibu Mkuu Wizara Dkt. Zainabu Chaula, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kujituma katika kutekeleza majukumu yao.

“Kila mmoja hapa ana karama yake, sasa tuunganishe hayo Maarifa ya mtu mmoja mmoja tutembee pamoja” Dkt. Chaula

Ameongeza kuwa, kiongozi ni wasifu katika eneo analofanya kazi na kuleta matokeo chanya kwenye eneno la utekelezaji wa majukumu yao hivyo, ni vyema watahakikisha wanatumia vipawa vyao kusadia kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

“Tutumie ujuzi na uwezo wote tulionao kuhakikisha tunasaidiana katika kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi na ufasaha ili kuhakikisha yanaleta matokeo chanya” alisema Dkt. Zainabu Chaula.

Kwa upande wake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. John Jingu amewashukuru Watumishi wa Wizara hiyo Mpya kwa ushirikiano waliompa wakati akitekeleza majukumu yake na kuwaasa kuendelea kuwapa ushirikiano viongozi wapya katika utekelezaji wa majukumu waliyopewa na Rais.

“Nawaahidi nitaendelea kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yenu tuendelee kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi ili tuendelee kumsaidia Rais katika kutatua changamoto za kimaendeleo “ alisema Dkt. Jingu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju, amewaasa watumishi kupendana na kushirikiana kwa pamoja katika majukumu yao ili kuwasaidia Viongozi kuendeleza jukumu la Maendeleo.

Mapema Januari 8, 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, aliunda Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum na kisha kuteuwa Viongozi wakuingoza Wizara hiyo.

MWISHO.

Previous articleWANAOCHIMBA MCHANGA NA KUSABABISHA ATHARI ZA KIMAZINGIRA DSM WAONYWA
Next articleKONGANI YA VIWANDA KUJENGWA DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here