Home ENTERTAINMENTS DKT. ABAS: TUTAIONESHA DUNIA UTAMADUNI WETU KUTOKEA MOSHI

DKT. ABAS: TUTAIONESHA DUNIA UTAMADUNI WETU KUTOKEA MOSHI


Na: John Mapepele, MOSHI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, leo Alhamisi Januari 20, 2022, amekagua maandalizi ya Tamasha kubwa la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro.

Katika Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Januari 22, 2022, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Chifu, akitumia jina la Chifu Hangaya. 

“Maandalizi yanakamilika na tayari vikundi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huu vinaendelea na mazoezi na wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania wameendelea kuwasili hapa Moshi.

“Tamasha hili linafungua njia ya matamasha mengine ya Utamaduni  wetu kuendelea hapa nchini. 

Tunataka kutumia utamaduni na sanaa kuileta dunia na kuionesha dunia kile Tanzania ilichonacho,” amesema Dkt. Abbasi kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.

Tamasha hilo limeandaliwa na machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Chifu Frank Marealle na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Previous articleKITUO CHA MALEZI CHA MATUMAINI CHAPONGEZWA
Next articleWAZAZI MSHIRIKIANE NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIMU: PROF.KAMUZOLA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here