Home LOCAL DK. MPANGO KWENDA MALAWI LEO KUMUWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA SADC

DK. MPANGO KWENDA MALAWI LEO KUMUWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA SADC

DAR ES SALAAM.
Makamu wa Rais  Dk. Philip Mpango leo Jumatatu, Januari 10, 2022 anaondoka nchini kwenda Lilongwe nchini Malawi kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika keshokutwa Januari 12, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, imesema Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa , Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit) utakaofanyika kesho Januari 11, 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here