Home SPORTS AZAM FC YATINGA FAINALI MAPINDUZI CUP

AZAM FC YATINGA FAINALI MAPINDUZI CUP

Na: stella Kessy .

MABINGWA wa kihistoria kwenye Kombe la Mapinduzi, Azam FC leo wameibuka na ushindi kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi mbele ya Yanga kwa ushindi wa penalti.

Baada ya dakika 90 kamilika huku timu zote zikitoshana nguvu hivyo mshindi ametafutwa kwa kupitia mikwaju ya penalti.

Ilikuwa ni moja ya mchezo wenye ushindani mkubwa ambapo Azam FC wao waliweza kupachika penalti 9 kimiani huku Yanga ikifunga penalti 8.

Zile tano tano za mwanzo zilikamilika kwa kila timu kufunga jambo lililopelekea kuweza kuanza kupigiana penalti mojamoja.

Ngoma ilikuwa nzito kwa kipa Erick Johola kuweza kuokoa penalti sawa na Kigonya Mathias wa Azam FC lakini ni Yassin Mustapha aliweza kukosa penalti na kuifanya Azam kushinda penalti ya mwisho kupitia kwa Mudhathir Yahya.

Previous articleDK. MPANGO KWENDA MALAWI LEO KUMUWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA SADC
Next articleWAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA VIJANA WA DUNIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here