Home Uncategorized DC JOKATE MWEGELEO AZINDUA RASMI TUZO ZA WAJASIRIAMALI WA TWCC JIJINI DAR

DC JOKATE MWEGELEO AZINDUA RASMI TUZO ZA WAJASIRIAMALI WA TWCC JIJINI DAR

Na: Hughes Dugilo, DAR.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegeleo amewataka wanawake  kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika Majukwaa mbalimbali hapa nchini.

DC Mwegelo ameyasema hayo leo Januari 29,2022 akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kwenye  uzinduzi rasmi wa tuzo za Wafanyabiashara wanake Wenye Viwanda zinazoandaliwa na Chama Cha wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC) zitakazotolewa Machi 8 Mwaka huu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Duniani kote.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahili wa Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake wanapata fursa za kumiliki uchumi wao na kuwa na majukwaa mbalimbali yanayotumika kutoa Elimu, mitaji na fursa za masoko ndani na nje ya nchi.

“Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais wetu mpendwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa mchango mkubwa kwa makundi mbalimbali ya wanawake kuweza kumiliki uchumi wake, hivyo ni wakati wa wanawake kuthamini, kujipanga na kusonga mbele” amesema Jokate.

Amewataka wafanyabiashara kujitokeza kushiriki katika tuzo hizo kwa kujiandikisha kwa wingi kuanzia leo Januari 29,2022  baada ya kuzinduliwa.

Awali akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mercy Silla amemshukuru Rais Samia kwa kuyawezesha majukwaa mbalimbali ya wanawake nchi na kwamba kuwepo kwa majukwaa hayo yameipa fursa Taasisi hiyo kukutana na wanawake wengi katika Mikoa yote hapa nchini.

“Tunamshukuru sana Rais wetu  Mhe.  Samia Suluhu Hassan kwa kuturudishia majukwaa yetu ya wanawake na yeye mwenye analisimamia hili, kwakweli tumeanza kuona mwanga” amesema Mercy Silla.

Nae Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza amemshukuru DC Jokate Mwegeleo kufika kwenye hafla hiyo na kwamba ujio wake umeleta faraja kubwa kwa wanachama wao.

Picha  za mbalimbali katika hafla hiyo.

Previous articleNAIBU WAZIRI MARY MASANJA AZINDUA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UVIKO 19 KWA WATOA HUDUMA ZA UTALII DAR
Next articleMAGAZETI YA LEO J.PILI JANUARI 30-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here