Na: HERI SHAABAN.
MKUU wa Wilaya ya Ilala Ng ‘wilabuzu Ludigija na Maafisa wa Mazingira wanatarajia kuzindua Kampeni ya Usafi February mwaka huu na Askari wa Suma JKT kukamata daladala ambazo azijaweka vifaa vya kuifadhi takataka.
Mkuu wa Wilaya Ludigija aliyasema hayo katika kampeni endelevu za usafi zilizozinduliwa kata ya Vingunguti Dar es Salam.
“Naagiza kwa Watendaji Idara ya Usafi na Mazingira mwezi February mwaka huu tuzindue kampeni ya Usafi katika daladala ambazo awajaweka vifaa vya takataka zikamatwe na kuchukulia hatua kwa kutupa taka ovyo wakamatwe wapigwe faini “alisema Ludigija.
Ludigija aliagiza Askari kukamata daladala zote zisizo na vifaa vya kuifadhia takataka na kuzitoza faini .
Alisema kwa sasa Wilaya ya Ilala safi maeneo yote katikati ya Mji maafisa mazingira wameweka vifaa vya Takataka.
Ludigija aliwataka wananchi wa Ilala kujenga tabia ya kuwa wasafi katika mazingira yao kila wakati kwani usafi ni afya.
Ludigija aliwataka Wakazi wa Vingunguti Jimbo la Segerea wawe mabalozi wa mazingira katika maeneo yao ikiwemo kutoa Elimu ya usafi kila wakati
Aliwataka maafisa Afya na Watendaji kusimamia usafi katika maeneo yao kila kata ikiwemo kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Serikali ambayo yalitolewa na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Afisa Mazingira Halmashauri ya jiji la Dar es Salam Rajabu Ngoda alisema halmashauri ya jiji kwa siku wanakusanya takataka tani 1100 wanasafirisha tani 600 kwenda dampo ya Pugu Kinyamwezi.
Ngoda alisema Kampeni ya Usafi ni endelevu kila kata inazinduliwa mwisho wa mwezi ikiwemo kutoa Elimu kwa wananchi wote.
Mwisho