Na: Hughes Dugilo, DAR.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umeendelea na zoezi lake la kukutana na wananchi mbalimbali kwa Lengo la kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni siku ya tatu toka walipoweka kambi katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Katika siku ya leo Januari 28, 2022 jumla ya Majina ya Biashara 26 na Makampuni 7 yalisaliwa na baadhi yao kufanikiwa kupatiwa vyeti vyao pao kwa hapo.
Baadhi ya wananchi waliofanikiwa kuondoka na vyeti vyao wamezungumzia changamoto ya vishoka wanaofanya usajili kwa lengo la kujIpatia kipato kwa watu wasiofahamu namna ya kutumia mifumo ya BRELA na kuiomba Taasisi hiyo kuwafuatilia na kuwachukulia hatua za kisheria.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa cheti chake Armani Dior licha ya kuonesha furaha yake ya kusajili Biashara yake na kupatiwa Cheti chake papo kwa hapo ameiomba BRELA kuongeza Elimu kwa wananchi juu ya kutumia mifumo ya mtandao ili kuepukana na vishoka.
“Naiomba sana BRELA watusaidie kutoa elimu, hapa ukiangalia wengi walijaribu kusajili kwenye mtandao lakini kuna mahali walikwama, matokeo yake wale vishoka wanapata nafasi ya kufanya Biashara” amesema Dior.
Na kuongeza kuwa.
“Zoezi hili liwe endelevu wafike mikoani wakifanya mazoezi kama haya watawasaidia wananchi wengi, naamini wakitengeneza timu ya watu tofauti tofauti wakasambaa mikoani watu wengi watafaidika” Ameongeza Dior.
Aidha amewahimiza wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kutumia fursa hiyo kupata elimu itakayosaidia kuepukana na vishoka wa mitaani.
BRELA wapo kwenye viwanja ya Mlimani City kwa siku tano kuanzia Januari 26, na kufikia tamati siku ya Jumapili Januari 30, 2022. kukutana na wananchi mbalimbali kwa Lengo la kufikisha huduma zao kwa jamii na kutatua changamoto zinazoikabili.
Picha za wananchi mbalimbali waliojitokeza kupata huduma. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO).