Home SPORTS BMT YAKUTANA NA SHIMISEMITA JIJINI DAR

BMT YAKUTANA NA SHIMISEMITA JIJINI DAR

Na: Mwandishi wetu

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limekutana na kufanya kikao na viongozi wa Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA), kwa lengo la kujadili namna ya uendeshaji wa Shirikisho hilo pamoja na kurejesha mashindano ya SHEMISEMITA ili kuendelea kuboresha na kuimarisha afya za watumishi wa Serikali za Mitaa kupitia michezo nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 18 Februari, 2022 katika moja ya kumbi za uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo Afisa Maendeleo ya Michezo BMT Halima Bushiri amesema pia viongozi wa Shirikisho hilo wanapaswa kuzingatia suala la Utawala Bora kwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ili kupata uongozi mpya.

“hongereni kwa kuitikia wito na kuja katika kikao hiki muhimu, kikubwa ni kukumbushana majukumu yetu, ni muda mrefu sasa umepita hatujafanya mashindano pamoja na uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya, tumekuwa tukisisitiza suala la Utawala Bora kwa viongozi wa vyama vya michezo nchini, ni vyema wote tukazingatia suala hili kwa kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu ipasavyo,”amesema Halima.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa SHIMISEMITA Angelus Likwembe ameipongeza BMT kwa kuona umuhimu wa Shirikisho hilo na kufanya kikao cha kukumbusha majukumu yake pamoja na kupanga mikakati madhubuti ya kuendelea kukuza michezo nchini.

“kwanza kabisa niipongeze sana BMT kwa kuona umuhimu wa Shirikisho letu na kutuita kufanya kikao cha pamoja ili kutukumbusha majukumu yetu na kujadili namna ya uendeshaji wa Shirikisho pamoja na kurejesha mashindano ya SHEMISEMITA ambayo yanafaida kubwa kiafya kwa watumishi wetu waliopo katika Halmashauri mbalimbali nchini,”amesema Likwembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here