NA; STELLA KESSY.
ZANZIBAR imefanikiwa kung’ara katika mashindano ya Taifa Cup yaliyomalizika juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa,Dar Es Salaam.
Katika Soka wanaume Mkoa Mjini Magharibi ambao wamejipatia zawadi ya shilingi milioni tatu,medali ya dhahabu na.kombe, huku nafasi ya pili ikienda kwa Mara ambao nao wamepata medali ya shabq shilingi milioni mbili na Kombe na tatu ilemqliziwa na Ruvuma ilipata medali ya shaba, Kombe na shilingi milioni moja.
Kwa upande wa wanawake wa Arusha wzlitawazwa kuwa malkia wa mashindano hayo waliojipatia zawadibya Kombe,shilingi milioni tatu na medali ya dhahabu, ikifuatiwa na Dar Es Salaam wakikamata nafasi ya pili kwa kupata zawadi ya shilingi milioni mbili,medali ya fedha na Kombe,huku Mara wakimalizia nafasi ya tatu wakipata medali ya shaba,Kombe na shilingi milioni moja.
Katika Mchezo wa netiboli Mjini Magharibi walitwaa Ubingwa na kupata medali ya dhahabu,Kombe na shilingi milioni tatu ,huku nafasi ya pili ikienda kwa Dar Es Salaam wakipata shilingi milioni mbili,medali ya fedha na Kombe ,ikimaliziwa na Dodoma nafasi ya tatu na waliojipatia zawadi ya shilingi milioni moja,medali ya shaba na Kombe.
Kwa mchezo wa riadha Kusini Unguja imeibuka na ubingwa ,huku nafasi ya pili ikienda kwa Arusha na ya tatu ikimaliziwa na Kilimanjaro ambao wamepata makombe.
Katika tasnia ya muziki wa singeli Mjini Magharibi imemaliza, nafasi ya tatu ,huku nafasi ya pili ikienda Dar Es Salaam na bingwa Morogoro,huku
Bongo flava wa tatu Dar Es Salaam ,akifuatiwa na Mbeya alichukua nafasi ya pili, na bingwa ni Pwani.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo Yusuph ,Singo,alisema kuwa wanamshukuru kwa kuanza na kumaliza salama mashindano hayo.
Alisema kuwa mikakati yao ni kuboresha zaidi mashindano hayo kwa kuongeza michezo ya kushindaniwa kwa wakati ujao.
Singo alisema kuwa kupitia mashindano hayo waajivunia kupata matunda yakiwamo na kurejesha michezo ya pamoja kwa kushirikiana kimuungano .
“Tunashukuru tumemaliza ,lakini kulikuwa na changamoto za hapa na pale na tumeweza kuchukua hatua,kwani mwaka ujao tunataka kuboresha zaidi,” alisema Singo.
Alisema kuwa wamefanikiwa kuibua na kuvumbua vipaji vipya,huku wanaamini vyama na mashirikisho ya michezo waleweza kuona vipaji ambavyo vitaweza kuingizwa kwenye timu za taifa na kuandaliwa kwa mashindano mbalimbali.
Mashindano hayo yalianza Desemba 10 mwaka huu yalifunguliwa na Waziri Utamaduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa na kufungwa na
Waziri wa Habari ,Vijana ,Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulid Mwita Desemba 16 mwaka huu.