Home SPORTS YANGA YAICHAPA PRISONS 2-1

YANGA YAICHAPA PRISONS 2-1


NA: STELLA KESSY

VINARA wa ligi kuu Yanga leo wameichakaza  Tanzania Prisons kwa mabao 2-1  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.

Hata hivyo Tanzania Prisons  ilitangulia kwa bao la Samson Mbangula kwa kichwa dakika ya 12 akimalizia mpira wa Kona wa Lambert Sabiyanka kutoka upande wa kushoto,

Katika  dakika za 23  Salum ‘Fei Toto’ akaisawazishia Yanga  kwa shuti kali baada ya kazi nzuri ya kiungo Khalid Aucho,katika dakika ya 43  kiungo Mrundi, Said Ntibazonkiza aliipatia bao timu yake.

Kwa ushindi huo, Yanga SC  inafikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa sasa na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao wamecheza mechi nane.

Kwa upande wa  Tanzania Prisons inayobaki na pointi zake nane za mechi tisa katika nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here