Home LOCAL WAZIRI WA MAMBO YA NJE BALOZI MULAMULA KUHUDHURIA MKUTANO WA AFRIKA NA...

WAZIRI WA MAMBO YA NJE BALOZI MULAMULA KUHUDHURIA MKUTANO WA AFRIKA NA UTURUKI INSTANBUL


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel  leo wamewasili Jijini Instanbul, Uturuki kwa ajili ya kushiriki kwenye Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi wa Afrika na Uturuki (Turkey – Africa Partership Summit) na kupokelewa na Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki Lut. Gen. Yacoub Hassan Mohamed.

Mhe Balozi Liberata MulaMula atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Viongozi wa Nchi unaotarajiwa kufanyika Tarehe 18 Disemba 2021 ukiwa na kauli mbiu ya Kuimarisha Ushirikiano kwa ajili ya Maendeleo.

Mkutano wa Viongozi wa Nchi utatanguliwa na Mikutano ya Mawaziri inayotarajiwa kufanyika Tarehe 17 Disemba 2021 ambayo itahusisha mkutano baina ya Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mkutano wa Mawaziri wa Afya ambapo wataangazia uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki katika kuboresha zaidi Sekta ya Afya nchini na mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Previous articleUJERUMANI YAIPONGEZA TANZANIA MAPAMBANO YA UVIKO-19, YAKABIDHI VIFAA TIBA VYA BILIONI 2
Next articleZANZIBAR YANG’ARA TAIFA CUP
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here