Home BUSINESS WATAKIWA KUTUMIA KAMPUNI ZILIZOSAJILIWA BRELA

WATAKIWA KUTUMIA KAMPUNI ZILIZOSAJILIWA BRELA

ARUSHA.

Wataalamu wa Ununuzi na ugavi hapa nchini wametakiwa kutumia kigezo cha kuhakiki uhalali wa kampuni zinazoomba zabuni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)wakati wa kufanya tathmini ya  kampuni hizo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA  Bw. Godfrey Nyaisa ametoa wito huo mapema leo  tarehe 2 Disemba, 2021, katika mkutano wa 12 wa Wataalam wa Ununuzi na Ugavi unaoendelea katika Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa(AICC) Jijini Arusha.

Bw. Nyaisa amesema kumekuwa na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya kampuni zinazotaka kufanya kazi na Serikali hivyo ni muhimu kuthibitisha uhalali wake kabla ya kufanya maamuzi, hivyo ni  vyema kuweka kigezo cha uthibitisho wa kampuni husika  kutoka BRELA.  

“Kuna baadhi ya kampuni hufunguliwa baada ya  kusikia kuna kazi fulani inatafuta mzabuni  hivyo kampuni za aina hiyo zinaweza kuwa na changamoto katika utendaji kazi kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kazi husika, Wataalamu wa Ununuzi  na   ugavi hakikisheni kuwa kigezo cha taarifa   za kampuni kutoka BRELA kinaambatishwa,” amefafanua Bw. Nyaisa.

Bw. Nyaisa amesema  mbali na kupata kazi mbalimbali Serikalini kampuni zinaposajiliwa na BRELA  inakuwa rahisi kupata fursa za mikopo kutoka katika mabenki kwani mabenki hufanya uchunguzi wa kampuni inayohitaji mkopo  kwa kupata taarifa  za kampuni husika kutoka BRELA.

Amesema mpaka sasa BRELA  imekwishasajili kampuni 150,000 na mifumo ya usajili kwa njia ya mtandao inaendelea kuboreshwa ili kuondoa changamoto ndogondogo zinazojitokeza wakati wa usajili kwa njia ya mtandao.

Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano.

Previous articleUTENDAJI WA MADAWATI YA KIJINSIA WAENDELEA KUIMARIKA – DKT. GWAJIMA
Next articleRC SENYAMULE AKAGUA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA GEITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here