Home BUSINESS WANANCHI MBALIMBALI WAPONGEZA WIZARA YA MADINI KWA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO ZANZIBAR

WANANCHI MBALIMBALI WAPONGEZA WIZARA YA MADINI KWA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO ZANZIBAR


Wananchi wa Zanzibar wanaotembelea mabanda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake wamepongeza huduma ya elimu inayotolewa na wataalam kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake hususan namna ya kuomba leseni za madini, kuchimba na biashara ya madini.

Pongezi hizo wamezitoa katika maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Maisara, Zanzibar ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara na Tume ya Madini, Jason Fernandes  amesema kuwa elimu waliyoipata kutoka kwenye banda hilo imewapa uelewa mpana kuhusu namna ya kuanza shughuli za uchimbaji wa madini kwa kuomba leseni, kuchimba na biashara ya madini.

“Watu wengi wenye nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini wamekuwa na hofu ya kujiingiza kwenye uchimbaji na biashara ya madini kutokana na kutokuwa na uelewa wa namna ya kujiingiza kwenye shughuli hizo, lakini elimu tuliyoipata kwenye banda la Tume ya Madini imetufungua macho na sasa tutaanza kuomba leseni za madini,” amesema Fernandes

Katika hatua nyingine ameomba maonesho kuendelea kufanyika mara kwa mara ili kutoa elimu kwa wananchi wengi zaidi kuhusu fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini na kuchangamkia ili kujiingizia kipato.

Naye Abdulaziz Mohamed ambaye ni mkazi wa Zanzibar sambamba na kupongeza kwa elimu nzuri iliyokuwa inatolewa na wataalam ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kufanya utafiti wa madini Zanzibar ili wananchi waweze kuchimba huku wakiwa na uhakika wa madini yanayopatikana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here