Home LOCAL WANANCHI KIJIJI CHA NJINJO KILWA WALILIA KITUO CHA AFYA

WANANCHI KIJIJI CHA NJINJO KILWA WALILIA KITUO CHA AFYA

Mwajuma Abdalla mkulima wa kijiji cha Njinjo akizungumza namna walivyotumia nguvu zao kuandaa eneo la kujenga kituo cha afya katika kijiji cha njinjo na mshangao wa kuchelewa kwa ujenzi huo.

Juma Mungutwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari .hawapo pichani wakilalamikia ucheleweshaji wa ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha njinjo.

Na: David John, KILWA

WANANCHI wa kijiji cha Njinjo kilichopo kata ya Njinjo Tarafa ya Njinjo wilayani Kilwa Mkoani Lindi wamelalamikia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuchelewesha ujenzi wa kituo cha afya ndani ya kijiji hicho.

Wananchi hao wakizungumza mbele ya waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa mwaliko wa wananchi hao jana walisema Novemba 3 mwaka huu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Wiston Kilangwa alifika kijijini hapo na kuwataka wananchi kujitolea kwa lengo la kuandaa eneo la kujenga kituo cha afya.

Walisema kuwa licha ya ujenzi wa kituo hicho lakini ujenzi wa karo la kuhifadhi maji pamoja na sehemu ya kuhifadhi vifaa vitakavyotumika katika ujenzi wa huo nakwamba cha kushangaza hadi kufikia leo hakuna kinachoendelea.

Akizungumza kwaniaba ya Wananchi wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Muhidini Matwiko alisema wanasikia kwamba ujenzi wa kituo hicho hautofanyika kijijni hapo  huku wakijua fika wananchi wametumia nguvu zao kufyeka eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho..

“Tunamuomba Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kilwa. Kufika kijijini hapa ili kutoa tamko la kuwaeleza wananchi kwamba wapi kituo kitajengwa kwani kujitokeza kwake kutaondoa stofahamu ambayo imejitokeza.” amesema Matwiko

Naye Mwananchi Juma Hassan Mungutwa.akizungumza katika mkutano huo wa wananchi alisema ujenzi wa kituo hicho ukifanywa katika kijiji cha njinjo ni halali kwakuwa kijiji hicho vijiji jirani vinapata huduma muhimu katika kijiji hicho.

Amefafanua kuwa  katika serikali ya awamu ya pili chini ya mzee ruksa .Ally Hassan Mwinyi alijenga kituo katika kijiji hicho hivyo kituo kikiendelea kubaki hapo hakuna tatizo .

“Ndugu mwandishi ujenzi wa kituo hiki hapa ni agizo la rais Samia Suluhu ambapo ametoa shilingi milion 250 iki kukamilisha ujenzi wa kituo hiki cha afya.”amesisitiza .Mwajuma Abdallah.

Ameongeza kuwa kuna sitofahamu kabisa juu ya kituo hicho cha afya na wanasikitika mno kutokana na kupoteza nguvu zao katika kusafisha eneo  hilo kwa ajili ya kuweka au kujenga kituo cha afya kama ilivyokuwa imeamuliwa .

Hata hivyo akijubu malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya kilwa Farida…  akizungumza kwa  njia ya simu ya kiganjani kutoka Kilwa amesema eneo hilo linahistoria yake lakini kwa kifupi kupitia kikao cha kamati ya maendeleo ya kata walikubaliana kama kituo cha afya kijengwe Njinjo.

Amesema baada ya hapo wananchi waliandaa eneo husika na hata ofisi ya Mkurugenzi ilitambua hilo na hata hivyo serikali iliungiza sh Milioni 250kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya ambapo fedha hizo zilikuwa zinakwenda huko ,lakini baadae mkurugenzi alitoa taarifa kwamba amepokea taarifa kutoka mkoani mchakato wa kituo hicho usimame hadi watakapopewa maelekezo.

Mwenyekiti amefafanua kuwa baada ya muda akapokea tena taarifa kutoka kwa mkurugenzi kwamba amepokea taarifa kwamba kituo hicho kinahama kutoka njinjo nakwenda kujengwa kijiji cha kipindimbi hivyo wanakwenda katika kikao mwishoni mwa wiki watapata taarifa zaidi.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here