Home ENTERTAINMENTS WANAMITINDO 15 KUTAMBA NDANI YA JUKWAA LA RUNWAY BAY 2021

WANAMITINDO 15 KUTAMBA NDANI YA JUKWAA LA RUNWAY BAY 2021



NA: MWANDISHI WETU

WANAMITINDO 15 kisiwani Unguja, wamechaguliwa kunadi mavazi ya wabunifu mbalimbali katika tamasha  la mitindo Runway Bay ambalo linafanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Usahili huo umefanyika leo, katika hoteli ya Marumaru na kuhudhuriwa na watu mbalimbali pamoja na wanamitindo 50 waliojitokeza kuwa nia nafasi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa usahili huo muandaaji wa tamasha hilo Waiz Houston Shelukindo, amesema mwaka huu jukwaa litakuwa na ukubwa wa mita 200 kitu ambacho hakijawahi kutokea hapa nchin.

“Moja ya mabadiliko tuliofanya mwaka huu ni kuongeza urefu wa jukwaa ili kumpatia mwanamitindo uwezo wa kuonyesha mavazi na madaha ila pia kuonyesha uhodari wa wabunifu katika kutengeneza mavazi yao,” anasema Waiz.

Aliongeza kuwa Zanzibari ndio kitovu cha tasnia ya mitindo na utalii katika bara la Afrika ndio sababu ameamua kuwekeza  katika tasnia hii.

“Zanzibari tunabahati kubwa hapa ndipo soko la mitindo lilipo nimepata nafasi ya kutembelea nchi tofauti nikagundua soko lipo hapa ndiyo maana nilipata njozi ya kuanzisha jukwaa hili kwa ajili ya kukuza na kuibua vipaji zaidi.”

Katika usahili huo majaji walikuwa wanamitindo mashuhuri hapa nchi G Taiga, Chied Adore, Khalid Balala, mbunifu kisiwani humo Magdy Stylesh.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni Utamaduni si ushamba,  tamasha linatarajiwa kufanyika Desemba 26 mpaka 29  katika barabara ya Mizingani pembezoni mwa bahari ya Hindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here