Home LOCAL WALIMU WAKUU NYASA WAPEWA MAFUNZO YA UDHIBITI UBORAWA SHULE

WALIMU WAKUU NYASA WAPEWA MAFUNZO YA UDHIBITI UBORAWA SHULE

 

NYASA.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas tarehe 16.12.2021, amefungua mafunzo ya uthibiti ubora wa shule wa ndani yenye lengo la, kuwajengea uwezo walimu wakuu pamoja na maafisa Elimu Kata kuthibiti ubora wa Shule katika Shule zao.

Mafunzo haya yanafanyika katika Kituo cha walimu kilichopo katika Shule ya Msingi ya mchepuo wa Kiingereza Lovund Wilayani hapa.

Akifungua mafunzo hayo, amewataka walimu hao Kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia kanuni za Utawala bor,a ikiwa ni pamoja na Uwazi na ushirikishwaji jamii hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kufahamu jamii inategemea kujifunza kutokana na walimu, kwa kuwa walimu ni kioo cha jamii.

Ameongeza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kufanya uthibiti wa nadani wa shule hivyo wanatakiwa kuyaelewa mafunzo hayo ili waweze kufanya uthibiti wa shule kwa kuwa walimu wakuu na Maafisa Elimu kata, ni Viongozi katika maeneo yao, hivyo kama watafanya uthibiti katika shule zao mafanikio makubwa yanakwenda kupatikana ikiwa ni pamoja na kuthibiti utoro na kuongeza ufaulu katika shule zao.

Kanali Thomas ametoa Wito kwa walimu kuhakikisha wanafundisha kwa bidii na kuwajengea uwezo wanafunzi ili waweze kupata mafanikio ya kitaaluma na kuendelea na masomo kati ngazi zingine za elimu.

“Ndugu walimu nyie ni viongozi katika maeneo yenu,mpo hapa kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili muweze kufanya uthibiti katika maeneo yenu kama matafanya uthibiti hakika mafanikio mbalimbali yatapatikana katika maeneo yenu na Wilaya kwa Ujumla.

Awali akitoa taarifa ya Mafunzo Mthiti Ubora wa Shule Wilayani hapa bw Blancer Luambano Amesema hii ni awamu ya pili ya utoaji mafunzo na wengine tayari walishapata mafunzo hayo na mafunzo hayo ni ya siku tatu ambayo yatawajengea uwezo wa kufanya uthibiti katika maeneo yao.

Mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here