Na: HERI SHAABAN (ILALA )
WAHENGA ALUMINUM wameishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutenga darasa la shule za madarasa ya awali kwa ajili ya Wanafunzi kuwandalia mazingira bora ya elimu .
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wahenga Aluminum John Ryoba leo,wakati wa mahafali ya Kituo cha Day Care CHADASH kilichopo Kinyerezi Kibaga Wilayani Ilala .
“Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwekeza katika sekta ya elimu na Sera ya Serikali ya elimu bila malipo kazi nzuri Serikali imefanya ,naishauri Serikali iwawekee watoto Msingi imara katika sekta ya elimu kwa kuanzisha shule za awali nchi zima “ alisema Ryoba
Mkurugenzi wa Wahenga Ryoba alisema watoto wanapoanzia madarasa ya awali inawajengea kujiamini pamoja na maadili mazuri darasani hivyo wazazi wawapeleke watoto madarasa ya awali kabla elimu ya Msingi.
Ryoba alisema watoto wanapoanzia darasa la awali wanakuwa na msingi imara wa kuwaongoza darasani mpaka chuo kikuu .
Akizungumzia Kituo cha Day Care Chadash Ryoba alisema amewapongeza Kituo kina mazingira bora amewataka wawekeze katika elimu ya Msingi mpaka chuo kikuu ili watanzania wasome katika chuo hicho na wageni mbalimbali.
Alisema Taifa lolote liweze kusonga mbele na kuwa na Maendeleo lazima watu wake wasome na kupata elimu bora sio bora elimu amewataka wadau kuwekeza katika elimu
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Day Care CHADASH Kokwihukya Kaino alisema Chadash Day Care ilianzishwa mwaka 2020 na kusajiliwa na Serikali kwa sasa ina Wanafunzi 25.
Mkurugenzi wa CHADASH Day Care alielezea changamoto za barabara mpaka kufika eneo hilo shule hiyo ameomba Serikali iwaboreshee miundombinu.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Kibaga Hashimu Kulana amewataka Wazazi kuzingatia katika sekta ya elimu kwa kusomesha watoto kuanzia elimu ya Msingi mpaka chuo Kikuu .
Mwenyekiti Hashimu alisema Wazazi wasio na uwezo ofisi yake ya Serikali za Mitaa itagharamia vifaa vya shule kwa Wanafunzi wa Mtaa Kibaga.
Mwisho