Home SPORTS WACHEZAJI WANNE AZAM FC KUIKOSA MECHI YA KAGERA SUGAR

WACHEZAJI WANNE AZAM FC KUIKOSA MECHI YA KAGERA SUGAR

 

Na: stella Kessy, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Azam fc umesema kuwa katika mchezo wa Kagera Sugar utawakosa wachezaji wanne ambao wanasumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Kwa taarifa iliyotumwa katika mtandao wao umesema kuwa wachezaji jumla ya wachezaji wanne  hawapo sawa na wataukosa mchezo wao dhidi ya Kagera.

Wachezaji ambao wataukosa mchezo huo moja wapo ni  mlinda mlango wao Mathias Kigonya, hatokuwepo katika mchezo sababu  alibainika kuwa na Malaria.

Huku Winga  Ayubu Lyanga, ambaye alifanyiwa upasuaji kutokana na mipasuko mitatu kwenye mifupa ya juu ya mdomo (maxila bone) inayofahamika kitaalamu kama lefort 1, 11 na 111), pia kuvunjika meno, anaendelea na mapumziko hadi Disemba 31.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kuanzia Januari Mosi mwakani, ataanza mazoezi mepesi ya viungo (gym) na anatarajiwa kurudi uwanjani rasmi kuanzia Januari 17, mwakani.

Lyanga aliumia Novemba Pili, mwaka huu dimbani Azam Complex kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold FC.

Pia winga wetu mwingine, Idd Seleman ‘Nado’ ambaye aliumia goti la kulia kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Novemba 30 mwaka huu dimbani Azam Complex, jana Jumatano alifafanyiwa kipimo cha MRI ili kujua ukubwa wa tatizo linalomkabili.

Beki wetu Lusajo Mwaikenda ambaye aliumia kwenye ajali ya barabarani, anatarajiwa kurejea rasmi kwenye mazoezi ya kawaida na wenzake muda wowote kuanzia sasa.

Lusajo amekuwa akifanya mazoezi mepesi ya peke yake, katika kipindi hiki anachouguza majeraha yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here