Home SPORTS VIINGILIO MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA Vs YANGA VYATANGAZWA

VIINGILIO MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA Vs YANGA VYATANGAZWA

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

ZIKIWA zimebaki siku 5 kabla ya mechi ya watani kati ya simba na Yanga  utaopigwa Disemba 11 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, tayari klabu hiyo imeweka viingilio vya mashabiki kwenda kucheki mtanange huo.

Viingilio vimepangwa sh 5000 kwa viti vya kijani,viti vya bluu na chungwa  sh.7000 VIP C sh 15000,VIP B 20,000 na VIP A sh 30,000.

Tiketi tayari zimeanza kuuzwa kupitia mitandao ya simu ili kuondoa usumbufu kwa mashabiki siku ya mechi.

Hata hivyo aliongeza kuwa mashabiki kutoka katika mikoa mbaimbali  watapata tiketi kupitia kwenye Ofisi zote za TTCL zilizopo karibu nao.

Simba ndio wenyeji wa mechi hiyo dhidi ya Yanga

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here